Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim: miwili inatosha

Muktasari:

  • Amorim ambaye amekuwa kocha wa sita mpya ndani ya timu hiyo katika kipindi cha miaka 11, amesisitiza yeye ni “mtu sahihi” wa kuifundisha Man United kwa sasa.

Manchester, England: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amesema ikiwa hatopata mafanikio ndani ya miaka miwili basi ataondoka kwenye timu hiyo.

Amorim ambaye amekuwa kocha wa sita mpya ndani ya timu hiyo katika kipindi cha miaka 11, amesisitiza yeye ni “mtu sahihi” wa kuifundisha Man United kwa sasa.

“Ndani ya miaka miwili mtajua kama mimi ni mtu sahihi kuwa kwenye kiti hiki au laa. Najua ikiwa uko Manchester United lazima ushinde mechi, hivyo sitawaambia nahitaji muda mrefu.” 

Kocha huyo wa zamani wa Sporting Lisbon, anaamini mabosi wa timu hiyo watajua hivi karibuni kabla hata ya miaka miwili kupita wamechagua mtu sahihi.

“Naamini mimi ni mtu sahihi kwa wakati sahihi. Nadhani tuna mawazo sawa mimi na viongozi, mtindo sawa na hiyo inaweza kusaidia. Naamini kwa wachezaji pia wanawaza kila ninachowaza. Nadhani tuna nafasi ya kuboresha na nataka kujaribu mambo mapya.  Nyinyi mnafikiria haiwezekani, lakini mimi nafikiri inawezekana.” 

Amorim atasimama katika mechi yake ya kwanza kama kocha wa Man United leo dhidi ya Ipswich. 

“Hii ni Manchester United, unahisi uzito wa historia licha ya timu kutopata mafanikio ndani ya miaka michache iliyopita na nahitaji kuwa sehemu ya historia hiyo,  ni kazi ngumu na najua kutakuwa na ugumu lakini naamini tutafanikiwa,” alisema Amorim ambaye  pia alielezea namna anavyoweza kufanya ili timu hiyo icheze kwenye staili ambayo anaihitaji.

“Kitu cha kwanza, nadhani tunapaswa kuwa wachezaji  bora zaidi. Hicho ni kitu tunachoweza kutambua baada ya kuona takwimu za kila mchezaji. hapa tutaangalia data za wachezaji kuanzia kasi na uhimili wao wa kukimbia na mambo mengine ya kimwili.”

“Mbali yakuwa sawa kimwili pia tunahitaji wachezaji watakaokuwa na akili ya mpira kwa sababu hauwezi kukimbia muda wote uwanjani lazima uwe na mipango ili uweze kushambulia na kufanya shinikizo kwa wapinzani wako, pia nadhani moja kati ya madhaifu yetu ni kupoteza mpira kwa haraka, huwa tunaitafuta na kupoteza kwa haraka sana jambo ambalo ni baya. Hiki ni moja kati ya vitu tunavyokwenda kuvifanyia kazi,” alisema Amorim.