Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim kugeukia madogo Man United

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Ripoti zilidai kwamba Man United ilijiandaa kuingia sokoni kwenye dirisha la Januari kufanya usajili wa kiungo ili kwenda kuiimarisha timu hiyo yenye maskani yake Old Trafford.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imefichua kwamba itahamia kwenye akademia yao kuchukua makinda wenye viwango bora wakati mastaa wa kikosi cha kwanza watakapokwenda kucheza michuano ya Afcon pamoja na kupata mbadala wa majeruhi Benjamin Sesko.

Ripoti zilidai kwamba Man United ilijiandaa kuingia sokoni kwenye dirisha la Januari kufanya usajili wa kiungo ili kwenda kuiimarisha timu hiyo yenye maskani yake Old Trafford.

Sesko amewekwa kando kwenye kikosi cha Slovenia katika mechi za kimataifa na atatakiwa kufanyiwa uchunguzi wa kina wa afya yake baada ya kushindwa kumaliza mechi ya Ligi Kuu England iliyopita ya sare ya 2-2 dhidi ya Tottenham Hotspur licha ya kwamba alitokea benchini.

Wakati maumivu ya goti yanayomsumbua Sesko yakiwa bado haijafahamika ni makubwa kiasi gani, kocha wa Man United, Ruben Amorim ana mchezaji mmoja tu, Joshua Zirkzee kwenye eneo la mshambuliaji wa kati.

AMO 02

Na Zirkzee, ambaye Amorim hamtazami kama Namba 9, ni mshambuliaji pekee aliyebaki benchini dhidi ya Spurs huku Mason Mount akipewa kipaumbele cha kucheza mechi hiyo.

Fowadi wa Kidachi hajafunga bao kwenye Ligi Kuu England kwa karibu miezi 12, mara ya mwisho alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa 4-0 dhidi ya Everton msimu uliopita.

Na tangu wakati huo, ameanzishwa kwenye mechi tisa tu. Zirkzee anatazamiwa kulazimisha uhamisho kwenye dirisha la Januari ili kwenda kupata nafasi ya kucheza huko kwingineko ili ajihakikishie namba kwenye kikosi cha Uholanzi kitakachokwenda Kombe la Dunia 2026 huko Amerika.

Lakini, kutokana na Sesko kuumia, hilo linazuia Zirkzee kufunguliwa mlango wa kutokea hiyo Januari. Sambamba na hilo, Man United itawakosa pia mastaa wake Bryan Mbeumo na Amad Diallo watakaoenda kwenye Afcon huko Morocco, michuano itakayoanza Desemba 21 hadi Januari 18. Noussair Mazraoui, naye atakwenda kwenye fainali hizo za Afcon kuichezea Morocco.

AMO 01

Hilo litatoa nafasi kwa makinda wa kutoka kwenye akademia kupandishwa kwenye kikosi cha kwanza kuja kuziba mapengo ya watakaoenda Afcon na majeruhi Sesko.

Amorim anaweza kuiga mfano wa Sir Alex Ferguson alipogeukia makinda baada ya kuwauza mastaa kadhaa ikiwamo Paul Ince, Andrei Kanchelskis na Mark Hughes baada ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England mfululizo.

Nahodha wa zamani wa Liverpool, Alan Hansen, amesema “huwezi kushinda chochote na watoto† alizungumza hilo wakati Man United ilipopoteza mechi ya kwanza ya msimu wa 1995/96 dhidi ya Aston Villa.

Lakini, Ferguson aliendelea kubaki na makinda wake na timu ikabeba ubingwa ikiwa na kikosi kilichosheheni makinda wa maana kama Gary Neville, David Beckham, Nicky Butt na Paul Scholes. Na sasa, Amorim makinda anaoweza kuwapa nafasi ni Chido Obi, Gabriele Biancheri, Shea Lacey, Jack Fletcher na Kobbie Mainoo.

Kuhusu usajili wa kiungo, Man United imelenga kumnasa mmoja wa mastaa hawa, Elliot Anderson, Carlos Baleba na Adam Wharton, lakini hilo linaweza kutokea kwenye dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi mwakani.