Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim kasema... hakuna kupoa

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Kocha Ruben Amorim bado anashikilia ratiba kali ya mazoezi na licha ya kuwepo kwa ratiba ya mechi za kimataifa ambayo nafasi ya kupumzika, aliwataka baadhi ya nyota wake ambao hawakuwa na majukumu ya timu za taifa aliendelea na ratiba ya kuwataka wachezaji wake kufanya mazoezi siku sita kwa wiki na kupumzika Jumatatu pekee.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United inashiriki mchuano mmoja tu wa Ligi Kuu England, lakini huko mazoezini ratiba yao ni kama inacheza michuano mingine mikubwa Ulaya.

Kesho Mashetani hao Wekundu wanashuka Uwanja wa Old Trafford dhidi ya Everton kusaka pointi tatu za kuwapandisha hadi nafasi za juu za ‘Top Four’ na ikianza kujipata, ratiba ya mazoezi inatajwa bado ni kali kama ya timu zinazoshiriki michuano zaidi ya miwili.

Kocha Ruben Amorim bado anashikilia ratiba kali ya mazoezi na licha ya kuwepo kwa ratiba ya mechi za kimataifa ambayo nafasi ya kupumzika, aliwataka baadhi ya nyota wake ambao hawakuwa na majukumu ya timu za taifa aliendelea na ratiba ya kuwataka wachezaji wake kufanya mazoezi siku sita kwa wiki na kupumzika Jumatatu pekee.

Taarifa zinaeleza Amorim ameamua kufanya hivyo ili kuhakikisha timu yake inakuwa tayari muda wowote baada ya kufanya vibaya sana msimu uliopita.

AMO 01

Amorim pia amefunguka, muda wa ziada ambao anautumia kuwafanyisha mazoezi wachezaji huwa ni kwa ajili ya kuingiza zaidi falsafa na mifumo yake kwenye vichwa vyao.

Kocha huyu pia amesisitiza muda mwingi hupendelea kuwaelekeza wachezaji wakiwa kiwanjani badala ya vyumbani.

“Nilikuwa mchezaji wa mpira wa miguu. Video zenye zaidi ya dakika 12? Sahau ni ngumu sana wachezaji kuangalia na kuwa na umakini, hivyo badala ya kujifungia ndani na kutazama video, huwa tunakwenda kiwanjani na baadae kutazama video kidogo.”

AMO 02

Wapinzani wa Man  United katika nafasi za juu wote msimu huu wanacheza michuano ya Ulaya jambo ambalo kwa namna fulani linapunguza mzigo kwa Man United ambao licha ya kufanya mazoezi kwa ratiba ileile, huwa wanapata muda mwingi wa kupumzika.

Man United ilikosa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupoteza fainali ya Europa League dhidi ya Tottenham msimu uliopita.

“Nadhani hatukuwa tayari kucheza michuano ya Ulaya,” alisema Amorim mwanzoni mwa msimu huu. “Hivyo ndivyo ninavyoona, kwangu nafikiri ili kuchez aligi hiyo tunahitaji muda zaidi wa kujenga timu yetu.”