Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim avunja TV, mashabiki wafurahia

Muktasari:

  • Kinachoelezwa ni Amorim alikasirishwa na kwa hasira hizo aliripotiwa kuvunja televisheni ya kufundishia baada ya kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Brighton uwanjani Old Trafford. Lisemwalo ni televisheni hiyo ilitumika kuwaonyesha wachezaji mbinu za mchezo kabla ya mechi.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amevunja televisheni kwenye vyumba vya kubadilishia baada ya kupata hasira akiwagombeza wachezaji wake kutokana na kucheza kwa kiwango cha ovyo kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Brighton, Jumapili iliyopita.

Kinachoelezwa ni Amorim alikasirishwa na kwa hasira hizo aliripotiwa kuvunja televisheni ya kufundishia baada ya kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Brighton uwanjani Old Trafford. Lisemwalo ni televisheni hiyo ilitumika kuwaonyesha wachezaji mbinu za mchezo kabla ya mechi.

Ripoti zinadai wachezaji walishtushwa na hasira za Amorim ambaye mara nyingi amekuwa kimya mechi zinapomalizika.

Amorim mara zote amekuwa akichagua kuwa kimya baada ya mechi kumalizika akijaribu kufanya uchambuzi wa mchezo uliopita na kujiandaa na mechi zijazo.

Mashabiki wa Man United wanaonekana kufurahishwa na hasira hizo za kocha kwa sababu zimelenga katika kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri.

Kwenye mitandao ya kijamii, shabiki mmoja aliandika: “Sijali Ruben Amorim amefanya nini kwenye vyumba vya kubadilishia baada ya mechi ya Brighton. Mimi namuunga mkono kwa 100%. Wachezaji wanapaswa kuamua kuipambania nembo.”

Shabiki mwingine aliongeza: “Hiki ndicho tunachohitaji. Wachezaji wanapaswa kuamka.”

Shabiki wa tatu alisema: “Safi. Yeye ni aina ya mtu anayehitajika na Man United kwa sasa. Dhamira na hasira ya kufanikiwa na kupambana. Nina uhakika mkubwa kwa Amorim kufikia mafanikio.” Shabiki wa nne alisema: “Zama mpya za Fergie. Sir Ruben Amorim”.

Kocha huyo Mreno mwenye umri wa miaka 39, alipozungumza na waandishi wa habari baada ya mechi, alisema Man United ya sasa imekuwa na kikosi cha ovyo katika historia ya klabu hiyo, aliposema: “Pengine hii ni timu ya ovyo zaidi katika historia ya Manchester United.”

Man United imekuwa na rekodi mbaya kwenye mechi za nyumbani kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 131. Kwenye msimamo wa ligi inashika nafasi ya 13 baada ya mechi 22, huku ikiwa juu kwa pointi 10 tu juu ya timu zilizopo kwenye shimo la kushika daraja na pointi 12 nyuma ya Top Four.