Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim atoa msimamo kuhusu mfumo mpya

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Bosi huyo Mreno amesema sasa hawezi kurudi kwenye fomesheni yake pendwa ya 3-4-3 hata kipindi ambacho wachezaji wake wote watakuwa wamerudi uwanjani.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amesema yupo tayari kubadilika.

Bosi huyo Mreno amesema sasa hawezi kurudi kwenye fomesheni yake pendwa ya 3-4-3 hata kipindi ambacho wachezaji wake wote watakuwa wamerudi uwanjani.

Amorim alibadilika na kupanga mabeki wanne kwa mara ya kwanza tangu alipochukua mikoba ya kuinoa timu hiyo miezi 13 iliyopita wakati alipopata ushindi wa 1-0 dhidi ya Newcastle United kwe-nye Boxing Day.

Na kocha huyo Amorim alitarajia kuendelea na mtindo wa kuchezesha mabeki wanne kwenye mechi dhidi ya Wolves iliyofanyika usiku wa kuamkia Jumatano. Jambo hilo limekuja kwa ghafla baada ya kocha huyo kuwahi kusema hata Papa hawezi kumshawishi kubadili fomesheni.

Lakini, alifanya mabadiliko ya kiufundi baada ya kuwakosa wachezaji saba kwenye mechi dhidi ya Newcastle United, huku mechi ya Wolves alitarajia kuwakosa wachezaji wanane.

Newcastle iliichapa Man United 2-0 uwanjani Old Trafford msimu uliopita na iliichapa tena 4-1 kwenye mechi ya marudiano. Amorim alikuwa na wasiwasi wa kupoteza tena kwenye Boxing Day, lakini mabadiliko ya fomesheni yalileta matunda mazuri na timu ikaibuka na ushindi.

Amorim amesema: “Ni mchakato. Nilipokuja hapa msimu uliopita, nilielewa kwamba kwa sababu sikuwa na wachezaji sahihi kwenye mfumo, lakini ule ulikuwa ni mwanzo wa mchakato.

“Tunajaribu kutengeneza utambulisho wetu. Kwa sasa mambo ni tofauti. Hatuna wachezaji wengi, hivyo inabidi kuzoee hali. Wachezaji wanaelewa kwanini tunabadilika.”