Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim ataka muda zaidi Man United

Amorim Pict

Muktasari:

  • Amorim ambaye amejiunga na Man United akichukua nafasi ya Erik ten Hag, licha ya kuamini yeye ni mtu sahihi amefunguka anajua madhara yatakayojitokeza kama hataweza kuanza kushinda michezo zaidi.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amesisitiza yeye bado ni mtu sahihi kuiongoza timu hiyo kwa muda mrefu licha ya kukumbana na rekodi zote mbovu za matokeo katika historia ya klabu hiyo.

Amorim ambaye amejiunga na Man United akichukua nafasi ya Erik ten Hag, licha ya kuamini yeye ni mtu sahihi amefunguka anajua madhara yatakayojitokeza kama hataweza kuanza kushinda michezo zaidi.

Man United walitolewa kwenye Kombe la FA na Fulham Jumapili ambao ulikuwa ni mchezo wa 10 kati ya 24 kwa Amorim kupoteza tangu ajiunge na wababe hao.

Kwa sasa Mashetani Wekundu hawa wanashika nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi Kuu wakiwa ni moja ya misimu yao mibovu zaidi katika historia yao.

Hadi sasa kombe pekee ambalo wanaonekana kuwa na uwezo wa kulipata ni Europa League ambalo wapo hatua ya 16 na jana walicheza mechi yao ya kwanza ya mtoano dhidi ya Real Sociedad.

Amorim alikiri mara mbili hivi karibuni kuwa hajui kama atakuwa Old Trafford kutimiza maono ya klabu ya kushinda Ligi Kuu ifikapo 2028.

Alipoulizwa kama yeye ni mtu sahihi wa kuiongoza mbele, Amorim alisema: "Hiyo iko wazi, najua ni nini cha kufanya. Lakini wakati mwingine kuna wasiwasi kwa sababu hatupati matokeo. Hivyo najua madhara yanayoweza kutokea pale unaposhindwa kushinda michezo. Nilikuwa na imani tangu siku ya kwanza ingawa mambo hayaendi vizuri kwa sasa, lakini bado nina imani."

Amorim alijiunga na Man United akitokea Sporting Lisbon Novemba mwaka jana lakini mashabiki wengi hivi karibuni wanaonekana kupoteza imani naye na wakikosoa zaidi mfumo wake wa 3-4-3 ambao yeye mwenyewe anaona hauna shida.

"Mfumo siyo tatizo, ni jinsi tunavyocheza kucheza."