Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim amrudisha Garnacho kundini

Muktasari:

  • Garnacho na Rashford wote wanajiandaa kuachana na timu hiyo dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi baada ya kutibuana na kocha huyo Mreno msimu uliopita.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amejiweka kwenye hatari ya kutibuana na Marcus Rashford zaidi baada ya kuripotiwa kumruhusu Alejandro Garnacho kufanya mazoezi na wenzake huko Carrington - wakati staa huyo wa England akitengwa, akitakiwa ajinoe kivyake.

Garnacho na Rashford wote wanajiandaa kuachana na timu hiyo dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi baada ya kutibuana na kocha huyo Mreno msimu uliopita.

Garnacho alipoteza nafasi yake kwenye kikosi mwishoni mwa msimu wa 2024-25, wakati alipowekwa kando na kocha Amorim katika mechi ya fainali ya Europa League dhidi ya Tottenham Hotspur, jambo lililodaiwa kutomfurahisha winga huyo wa Kiargentina.

Kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi, Garnacho amekuwa akihusishwa na Napoli na Chelsea, zikihitaji huduma yake. Lakini, staa huyo mwenye umri wa miaka 21, aliruhusiwa kufanya mazoezi ni wachezaji wenzake wakati hatima yake ikijadiliwa, kwa mujibu wa ESPN.

Alionyesha kiwango kizuri baada ya kufunga mabao 11 na asisti tisa, lakini bado halishindwa kuisaidia timu isimalize nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England. Kuna timu nyingi zinamtaka.

Lakini, kwa Rashford mambo ni magumu kwake. Fowadi huyo alitolewa kwa mkopo kwenda Aston Villa kwenye dirisha la Januari baada ya kocha Amorim kutofurahishwa na kiwango chake mazoezini na mwenyewe aliweka wazi yupo tayari kuhama.

Rashford sambamba na Garnacho na wachezaji wengine watatu, wamepewa muda zaidi wa likizo kutafuta timu za kwenda kuzitumikia, lakini walirejea Carrington, Jumatatu na Jumanne, wakifanya mazoezi kivyao. Rashford amekuwa akihusishwa na Barcelona wanaohitaji winga baada ya kumkosa Nico Williams, aliyeamua kusaini mkataba wa miaka 10 kubaki Athletic Bilbao.

Na kwenye hilo, Rashford yupo tayari kupunguza mshahara wake wa Pauni 325,000 kwa wiki ili ajiunge na Barcelona, ambayo inataka uhamisho wa mkopo, wakati Man United inataka ada ya Pauni 40 milioni. Rashford anafahamu wazi, hapa maisha tena Old Trafford endapo kama Amorim atabaki, huku jezi yake yenye Namba 10, ikikabidhiwa kwa supastaa wa Kibrazili, Matheus Cunha.

Wachezaji wengine walioambiwa watafute timu za kwanza ni Jadon Sancho, Antony na Tyrell Malacia.