Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim akiri kuiba ujuzi kwa wapinzani

Muktasari:

  • Man United ilipindua meza kipindi cha pili kwenye mechi yao dhidi ya Crystal Palace ilipotoka nyuma kwa bao 1-0 na kushinda 2-1 ugenini na ilikuwa mara yao ya pili kushinda kwenye mechi ya ugenini kati ya 12 za mwisho ilizocheza Ligi Kuu England.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amesema kwa kutania timu yake inaiba mbinu za kufunga mabao yatokanayo na mipira ya adhabu kutoka kwa wapinzani wao kwenye Ligi Kuu England.

Man United ilipindua meza kipindi cha pili kwenye mechi yao dhidi ya Crystal Palace ilipotoka nyuma kwa bao 1-0 na kushinda 2-1 ugenini na ilikuwa mara yao ya pili kushinda kwenye mechi ya ugenini kati ya 12 za mwisho ilizocheza Ligi Kuu England.

Joshua Zirkzee na Mason Mount walifunga mabao yao wakiwa wametofautiana dakika tisa tu, huku yote yakitokana na mipira ya adhabu iliyopigwa na Bruno Fernandes.

Kocha Amorim alimtaka msaidizi wake Carlos Fernandes kusimama kwenye eneo la ufundi kila kwenye tukio la upigaji wa mipira ya adhabu iwe dhidi yao au dhidi ya timu pinzani na Man United imeanza kupata faida, ikifunga mabao pia kwa njia ya mipira ya kona dhidi ya Tottenham na Nottingham Forest mwanzoni mwa mwezi Novemba.

Alipoulizwa kuhusu mipigo ya mipira ya adhabu ya Man United, Amorim alisema: “Tunajifua sana. Tunatumia muda mwingi sana, tunajifunza sana na tunajifunza mengi England. Nadhani mmeona mengi, lakini unapokuja kwenye Ligi Kuu England unajifunza mengi kutoka kwa timu nyingine kwa namna wanavyopiga mipira hiyo. Tumeiba vitu vingi ili kufunga mabao.â€

Crystal Palace ilikuwa haijapoteza mechi yoyote kati ya 12 ilizocheza nyumbani uwanjani Selhurst Park tangu Februari mwaka huu, lakini Man United ilishinda ikitokea nyuma ikiwa ni mara ya kwanza tangu ilipoichapa Athletic Bilbao 4-1 Mei mwaka huu.

Amorim alisema: “Niliona dakika 10 za mwisho katika kipindi cha kwanza wapinzani walikuwa wamechoka, hivyo nilijua watataabika pia kwenye kipindi cha pili. Tulikuwa na hiyo hisia ya kufanya kitu kubadili namna ya uchezaji wetu. Ilikuwa hivyo. Tulijaribu kubadilisha vitu ndani ya mchezo. Na Josh alikuwa kiunganishi wetu.”

Zirkzee alifunga bao lake la kwanza kwenye Ligi Kuu England baada ya siku 364 alipoisawazishia Man United kwenye dakika 54, huku akicheza mechi yake ya kwanza aliyoanzishwa kwenye Ligi Kuu England baada ya siku 225 alipocheza dhidi ya Everton, Jumatatu iliyopita. Mdachi huyo alirejea kwenye kikosi cha kwanza baada ya Matheus Cunha na Benjamin Sesko kuwa majeruhi na Zirkzee alilipa fadhila hiyo kwa kocha Amorim, alipofunga kwa mara ya kwanza tangu Aprili mwaka huu.