Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alonso: Trent benchi litamhusu sana

TRENT Pict

Muktasari:

  • Alonso alisema kuwa si jambo rahisi kumpa nafasi ya kudumu mchezaji mmoja pekee na kutokana na hilo Trent aliwekwa benchi katika mchezo uliopita dhidi ya Real Sociedad.

MADRID, HISPANIA: KOCHA wa Real Madrid, Xabi Alonso amesema beki wao, Trent Alexander-Arnold  itatakiwa azoee suala la kukaa benchi mara kwa mara kwa sababu ya ushindani uliopo kati yake na Dani Carvajal.

Alonso alisema kuwa si jambo rahisi kumpa nafasi ya kudumu mchezaji mmoja pekee na kutokana na hilo Trent aliwekwa benchi katika mchezo uliopita dhidi ya Real Sociedad.

"Kwa bahati nzuri, tuna ushindani mzuri ndani ya kikosi, na wachezaji wanacheza kwa umakini kwa sababu wenzao pia wako tayari muda wowote. Suala hili pia hutokea katika nafasi nyingine, kama beki wa kati au winga. Atakayestahili ndiye atakayepata nafasi ya kucheza; na hilo litakuwa la mara kwa mara msimu mzima."

Trent amekuwa akipitia wakati mgumu wa kuwekwa benchini mara kwa mara tangu ajiunge na Madrid katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa England alipata dakika tatu pekee za kucheza katika mchezo dhidi ya Real Oviedo katika mechi ya pili ya ligi ya Madrid msimu huu, kabla ya kurejea kikosini kwenye ushindi wa 2-1 nyumbani dhidi ya Real Mallorca.

Hata hivyo, kocha Xabi Alonso aliamua kumrejesha kikosini beki mwenye uzoefu Dani Carvajal Jumamosi alasiri katika mchezo wa Real Madrid dhidi ya Real Sociedad.

Carvajal ambaye ana uzoefu mkubwa, amekuwa chaguo la kwanza kwa Alonso katika siku zake za mwanzo kwenye viunga vya Bernabeu.

Alexander-Arnold anajulikana zaidi kwa uwezo wake wa kushambulia, lakini kwa sababu Real Madrid tayari ina washambuliaji wengi, Alonso ameamua kuzingatia zaidi uimara wa safu ya ulinzi.

Hali hii inampa Alonso changamoto ya kuamua ni lini amtumie Alexander-Arnold na ni lini ampe nafasi Carvajal.

Alexander-Arnold pia hakuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England wakati wa mapumziko ya ligi kupisha mechi za timu za taifa na kocha Thomas Tuchel alisema: "Nilizungumza na Trent. Ilikuwa simu ngumu, lakini nilitaka asikie kutoka kwangu moja kwa moja. Aliheshimu uamuzi wangu na alisema wazi kwamba ana hamu na ari kubwa ya kurejea katika timu ya taifa."