Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alonso atua! Apagawisha mashabiki Chelsea

ALONZO Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo raia wa Hispania aliteuliwa kuinoa Chelsea kwa mkataba wa miaka minne, akichukua nafasi ya Liam Rosenior, ambaye alidumu madarakani kwa siku 107 pekee kabla ya kuondolewa.

LONDON, ENGLAND: ENZI mpya zimeanza Chelsea baada ya kocha mpya, Xabi Alonso, kutua rasmi katika kituo cha mazoezi cha Cobham katika siku yake ya kwanza ya maandalizi ya msimu mpya, huku mashabiki wa klabu hiyo wakimkaribisha kwa shangwe na matumaini makubwa.

Kocha huyo raia wa Hispania aliteuliwa kuinoa Chelsea kwa mkataba wa miaka minne, akichukua nafasi ya Liam Rosenior, ambaye alidumu madarakani kwa siku 107 pekee kabla ya kuondolewa.

Alonso alianza rasmi majukumu yake Julai 1, lakini sasa ameonekana kwa mara ya kwanza akiwasili katika kituo cha mazoezi cha Cobham tayari kuanza kazi ya kuijenga timu kuelekea msimu mpya.

ALO 01

Katika video iliyosambazwa na Chelsea kupitia mitandao ya kijamii, Alonso alionekana akishuka kwenye gari akiwa ametulia na kubeba begi mgongoni kabla ya kuelekea ndani ya kituo hicho.

Chelsea iliambatanisha video hiyo na ujumbe uliosomeka: "Hapa ndipo kila kitu kinaanza... sura mpya inatusubiri."

ALO 03

Video hiyo iliwasisimua mashabiki wa Chelsea, ambao walifurika kwenye mitandao ya kijamii kumkaribisha kocha huyo wa zamani wa Real Madrid.

Shabiki mmoja aliandika: "Nimetabasamu na hata machozi yamenitoka. Mungu wangu!"

ALO 02

Mwingine alisema: "Huyu ndiye mtu wa wakati huu. Karibu kwenye klabu yetu, Bwana Alonso."

Shabiki wa tatu aliandika: "Amewasili! Sasa kazi ianze. Tunaamini msimu huu tutafurahia soka bora."

Mwingine aliongeza: "Amewasili, na ndiye kocha sahihi kwa Chelsea."