Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alonso anajua amtumie vipi Jude

ALONSO Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo wa zamani wa Liverpool ametua Bernabeu kwenda kurithi mikoba ya Carlo Ancelotti baada ya kupata mafanikio mazuri kwa miaka miwili aliyokuwa akiinoa Bayer Leverkusen ya Ujerumani.

MADRID, HISPANIA: KOCHA Xabi Alonso amefichua mipango yake juu ya namna atakavyomtukia kiungo Mwingereza Jude Bellingham baada ya kutambulishwa kuwa kocha mpya wa Real Madrid.

Kiungo huyo wa zamani wa Liverpool ametua Bernabeu kwenda kurithi mikoba ya Carlo Ancelotti baada ya kupata mafanikio mazuri kwa miaka miwili aliyokuwa akiinoa Bayer Leverkusen ya Ujerumani.

Alonso amerejea Hispania baada ya kuwahi kutamba kwenye La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati alipokuwa mchezaji wa Real Madrid kati ya mwaka 2009 na 2014.

Na sasa anarudi kwenye kikosi hicho cha Bernabeu kama kocha kufuatia kusaini mkataba wa miaka mitatu na imedaiwa anataka kuifanya Los Blancos kuwa timu isiyozuilika uwanjani.

Kama hilo ndivyo lilivyo, basi Bellingham atashuhudiwa akicheza kwenye kiungo ya kati. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 ametamba kwenye La Liga tangu alipojiunga na Real Madrid mwaka 2023 na kufunga mabao 23 na asisti 13 katika msimu wake wa kwanza, alipokuwa akicheza kiungo ya juu.

Staa huyo wa zamani wa Borussia Dortmund alishuhudia nafasi yake ikibadilika msimu huu baada ya ujio wa mshambuliaji Kylian Mbappe. Na msimu huu sasa amefunga mabao 14 na asisti 14.

Na Alonso alisema: “Bellingham yupo kwenye nafasi nzuri kufanya naye kazi. Namtazama kama kiungo. Tutazama kumfanya awe na faida kwa kadri inavyowezekana.

“Bellingham anaweza kuwa spesho kwenye kila eneo. Ni mchezaji wa aina ya kipekee. Ameonyesha kiwango kikubwa kwenye historia ya Real Madrid. Ana miaka 21 na ni silaha kubwa kwa klabu.”

Alonso aliulizwa pia namna atakavyoweza kupata huduma bora kutoka kwa Mbappe na Vinicius Jr kupitia mtindo wake wa uchezaji. Wachezaji hao wanatajwa kama tishio kwenye fowadi ya Real Madrid, lakini wamekuwa wakishindwa kuonyesha makali yaliyotarajiwa kwa msimu huu.

Na kwenye hilo Alonso alisema: “Ni baraka tosha kuwa na wachezaji wa viwango hivi. Si tu Kylian au Vinicius, bali na wengine pie ni wazuri. Ni wachezaji wa kuleta tofauti kwenye mechi, yatupasa kutafuta namna ya kuvuna huduma bora kutoka kwao.”