Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alisson aondolewa mtu wake Anfield

Alisson Pict

Muktasari:

  • Mbrazili huyo alikuwa kwenye kiwango bora sana msimu uliopita, alipocheza mechi 28 wakati Liverpool ikifanikiwa kunyakua taji la Ligi Kuu England.

LONDON, ENGLAND: KIPA, Alisson ameripotiwa kukuna kichwa kwa sasa huko Liverpool akiwaza itakuwaje baada ya kudaiwa kuwapo na mabadiliko makubwa kwenye idara ya makipa ya klabu hiyo.

Mbrazili huyo alikuwa kwenye kiwango bora sana msimu uliopita, alipocheza mechi 28 wakati Liverpool ikifanikiwa kunyakua taji la Ligi Kuu England.

Kipa, Alisson wasiwasi wake unakuja baada ya tangazo la hivi karibuni, kwamba kwenye idara hiyo ya makipa kuna mabadiliko yanakwenda kufanyika baada ya shujaa wake wa tangu utotoni, kipa wa zamani wa Brazil, Claudio Taffarel anaachana na miamba hiyo ya Anfield.

Kipa Taffarel, aliyeichezea Brazil mechi 101 na kudakia timu hiyo kwenye fainali mbili za Kombe la Dunia, akishinda ile ya 1994 - alijiunga kweye benchi la ufundi la Liverpool mwaka 2021 chini ya kocha Jurgen Klopp. Lakini, sasa baada ya ujio wa kocha mpya, Arne Slot, Taffarel analazimika kuondoka.

Alisson alikuwa kwenye wakati mzuri wakati alipokuwa chini ya Mbrazili mwenzake, mtu ambaye pia alikuwa akimhusudu tangu utoto wake, lakini sasa Taffarel anaondoka, kocha Slot analeta mtu wake.

Taffarel anaondoka na kocha mwingine wa makipa Fabian Otte, ambaye alikuja na Arne Slot dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana na kwamba sasa benchi hilo la makocha wa makipa litakuwa chini ya Xavi Valero, kipa wa zamani Wrexham, ambaye aliwahi kuwapo Liverpool katika kipindi cha kocha Rafa Benitez mwaka 2007, sasa anarudi Anfield baada ya miaka 15.

Valero anatua Anfield sambamba na Giovanni van Bronckhorst, ambaye alichukua nafasi ya msaidizi wa Slot baada ya John Heitinga kwenda Ajax kwenye dirisha hili la kiangazi mwaka mmoja baada ya kuwa na miamba hiyo ya Anfield.