Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AFCON sasa kila baada ya miaka minne

AFCON Pict

Muktasari:

  • Mashindano ya mwaka huu nchini Morocco yalisogezwa mbele kwa miezi sita baada ya FIFA kuanzisha Kombe jipya la Dunia la Klabu, ambalo lilifanyika Marekani katikati ya Juni na Julai.

ULE utamaduni wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kufanyika kila baada ya miaka miwili, unaenda kufa kutokana na mbadiliko yaliyofanywa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Michuano hiyo kwa sasa itaandaliwa kila baada ya miaka minne badala ya miaka miwili kutokana na mabadiliko hilo la CAF huku fainali ya mwaka 2029 zikirejeshwa kwa mwaka mmoja ili kuepusha zile za 2030 kuingilia na Fainali za Kombe la Dunia za 2030.

Uamuzi huo wa kushangaza ulifikiwa juzi Jumamosi katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya CAF kilichofanyika katika mji mkuu wa Morocco, Rabat na kutangazwa rasmi katika mkutano na waandishi wa habari na Rais wa CAF, Dk Patrice Motsepe.

Michuano hiyo inayokadiriwa kuingiza takribani asilimia 80 ya mapato ya CAF kwa kawaida yamekuwa yakifanyika kila baada ya miaka miwili tangu kuanzishwa kwake mwaka 1957.

Jana Jumapili ilianza rasmi kwa fainali za 35 la michuano hiyo kwa wenyeji Morocco kuvaana na Comoros katika mechi ya ufunguzi iliyopigwa kuanzia saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

afc 02

Motsepe amesema kuwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zilizopangwa kufanyika mwaka 2027 katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda zitaendelea kama ilivyopangwa, kisha michuano ijayo ya 2029 itafanyika 2028 na baada ya hapo fainali hizo zitakuwa likiandaliwa kila baada ya miaka minne.

Aidha, Motsepe alitangaza kuanzishwa kwa Ligi ya Mataifa ya Afrika (African Nations League) itakayokuwa ikifanyika kila mwaka kuanzia 2029, ili kuziba pengo hilo kwa kufuata mfano wa Ulaya ambako mashindano makuu hufanyika kila baada ya miaka minne.

“Kwa kihistoria, Kombe la Mataifa lilikuwa chanzo kikuu cha mapato kwetu, lakini sasa tutakuwa tunapata rasilimali za kifedha kila mwaka,” amesema Dk Motsepe na kuongeza;

“Ni muundo mpya unaosisimua ambao utachangia uhuru wa kifedha endelevu na kuhakikisha uratibu bora zaidi na kalenda ya FIFA.”

afc 01

Pendekezo la kuandaa Kombe la Mataifa kila baada ya miaka minne lilikuwa limewahi kutolewa na Rais wa FIFA, Gianni Infantino, lakini CAF ilikuwa imelipinga kutokana na utegemezi mkubwa wa mapato unaotokana na michuano hiyo.

Ratiba ya AFCON kwa muda mrefu imekuwa ikizua mjadala, kwani mara nyingi imekuwa ikifanyika katikati ya msimu wa Ligi za Ulaya, hali iliyozilazimu klabu kuwaachia wachezaji wa Kiafrika.

Mgongano huo wa maslahi ulitarajiwa kutatuliwa kwa kuhamishia mashindano katikati ya mwaka kuanzia 2019, lakini mashindano yaliyofanyika Cameroon 2021 na Ivory Coast 2023 yalirejeshwa tena mwanzoni mwa mwaka.

Mashindano ya mwaka huu nchini Morocco yalisogezwa mbele kwa miezi sita baada ya FIFA kuanzisha Kombe jipya la Dunia la Klabu, ambalo lilifanyika Marekani katikati ya Juni na Julai.