Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Achraf Hakimi ajiweka njia panda AFCON 2025

HAKIMI Pict

Muktasari:

  • Morocco, ambayo ilitolewa katika hatua ya 16 bora kwenye michuano iliyopita nchini Ivory Coast, inatajwa kuwa miongoni mataifa yanayopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Afrika mwaka huu.

Nahodha na beki wa pembeni wa timu ya taifa ya Morocco, Achraf Hakimi, yupo njia panda kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) zitakazofanyika nchini kwao, baada ya kuumia wakati wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Paris Saint-Germain (PSG) na Bayern Munich, Novemba 4, 2025.

Mshambuliaji wa Bayern Munich, Luis Díaz, alimtega vibaya Hakimi mwishoni mwa kipindi cha kwanza katika uwanja wa Parc des Princes, kwenye mechi hiyo na mwamuzi alimuadhibu Mcolombia huyo kwa kumuonyesha kadi nyekundu.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool mwenye umri wa miaka 28, alionyeshwa kadi ya njano mwanzoni, lakini baada tukio la kumtega Hakimi, uamuzi wa video (VAR) ulipendekeza adhabu kali zaidi, na Díaz akatolewa nje kwa kadi nyekundu.

Licha ya kuwa pungufu, Bayern ilihimili mashambulizi ya PSG katika kipindi cha pili na kushinda mechi hiyo kwa mabao 2–1, hivyo kuendelea kuwa na rekodi ya asilimia mia moja kwenye hatua ya makundi ya msimu huu.

HAKI 01

Mshambuliaji wa PSG, Ousmane Dembélé, ambaye alitoka uwanjani dakika ya 25 kutokana na jeraha la mguu wa kushoto (calf), atakuwa chini ya uangalizi wa matibabu kwa wiki kadhaa zijazo, kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo ya jijini Paris, Ufaransa.

Majeraha hayo kwa wachezaji hao wawili muhimu wa kikosi kilichoshinda mataji manne msimu uliopita ni pigo lingine kwa kocha Luis Enrique, ambaye bado anakabiliwa na majeruhi wengine akiwemo Désiré Doué (aliyepata jeraha la paja) na beki Nuno Mendes, aliyeumia goti la kushoto.

Hakimi, aliyeteuliwa kuwa nahodha wa Morocco mwishoni mwa mwaka 2024, anatarajiwa kuwa mmoja wa nyota wakutumainiwa kwenye fainali za AFCON, ambazo zitaanza Desemba 21, 2025 kwa mechi kati ya wenyeji dhidi ya Comoros. Tamati ya mashindano hayo yanayoshirikisha jumla ya timu 24 zikishindania ubingwa unaoshikiliwa na Ivory Coast, ni Januari 18, 2026.

HAKI 02

Morocco, ambayo ilitolewa katika hatua ya 16 bora kwenye michuano iliyopita nchini Ivory Coast, inatajwa kuwa miongoni mataifa yanayopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Afrika mwaka huu.

Wakati huohuo, gharama inayokadiriwa kufikia euro bilioni 2 kwa ajili ya ukarabati wa viwanja kwa AFCON na Kombe la Dunia 2030 (ambapo Morocco itashirikiana kuandaa na Hispania na Ureno) imezua utata mkubwa. Waandamanaji wanasema fedha hizo zingetumika kuboresha huduma za umma kama elimu na afya.