Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rafu ya Diaz yamliza Hakimi

Muktasari:

  • Miamba ya soka ya Ufaransa na mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, PSG ilikuwa uwanjani Parc des Princes kukabiliana na Bayern katika mechi iliyomalizika kwa Wajerumani hao ambao ni mabingwa wa Bundesliga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

PARIS, UFARANSA: BEKI, Achraf Hakimi ameangusha chozi baada ya kuchezewa rafu mbaya na Luis Diaz katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Paris Saint-Germain ilipomenyana na Bayern Munich.

Miamba ya soka ya Ufaransa na mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, PSG ilikuwa uwanjani Parc des Princes kukabiliana na Bayern katika mechi iliyomalizika kwa Wajerumani hao ambao ni mabingwa wa Bundesliga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Bayern ilitawala kipindi cha kwanza cha mchezo huo, ambapo Diaz, ndiye aliyefunga mabao yote mawili ya Bayern kabla ya kutolewa kwa kadi nyekundu kwa rafu yake mbaya.

Mambo yalikuwa magumu kwa PSG baada ya kumshuhudia staa wake Ousmane Dembele akilazimika kutoka uwanjani kwenye dakika ya 25 baada ya kuumia.

Diaz alitolewa kwa kadi nyekundu katika saba za majeruhi za kipindi cha kwanza baada ya kufanya jaribio la kutaka kumnyang’anya mpira Hakimi akitokea nyuma na kumsababishia maumivu makali mchezaji mwenzake kiasi cha kumfanya beki huyo kuangusha machozi.

Awali, mwamuzi wa mchezo alimwonyesha Diaz kadi ya njano, lakini baada ya picha za marudio za VAR, kadi hiyo ilifutwa na staa huyo wa Colombia kuonyeshwa nyekundu ya moja kwa moja.

Diaz alifunga bao lake la kwanza kwenye dakika ya nne kabla ya kuongeza jingine dk32, lakini sasa kadi nyekundu itamfanya akose mechi ijayo ya kuwakabili Arsenal baadaye mwezi huu.

Majeraha ya Hakimi yanatishia uwezekano wa kwenda kucheza michuano ya Afcon itakayoanza miezi michache ijayo. Staa huyo wa Morocco alicheza mechi hiyo akiwa anatimiza umri wake wa miaka 27, lakini mambo hayakuwa mazuri akihitaji watu kumsaidia kutoka uwanjani.

Morocco ndiyo itakayokuwa mwenyeji wa michuano ya Afcon na Hakimi ni nahodha wa kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo.

Kukosekana kwa Hakimi na Dembele kuliifanya PSG kushindwa kusawazisha katika mechi hiyo dhidi ya Bayern, ambapo bao lao la kujifariji lilifungwa na Joao Neves kwenye dakika ya 74 na hivyo kumpoteza mchezo huo kwa mabao 2-1 nyumbani mbele ya wababe wa Ujerumani.