Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diaz atupia mbili, aambulia kadi nyekundu Bayern ikiilaza PSG

Muktasari:

  • Timu hiyo ya Ujerumani imefikisha ushindi wa 16 mfululizo katika michuano yote, ikiwemo michezo minne ya ushindi katika Ligi ya Mabingwa, na inaongoza msimamo.

PARIS, UFARANSA: Mabao mawili ya Luis Díaz yameisaidia Bayern Munich iliyomaliza na wachezaji 10 kuendeleza mwanzo wao mzuri kwa kueashinda mabingwa watetezi wa Ulaya, Paris Saint-Germain (PSG).

Timu hiyo ya Ujerumani imefikisha ushindi wa 16 mfululizo katika michuano yote, ikiwemo michezo minne ya ushindi katika Ligi ya Mabingwa, na inaongoza msimamo.

Díaz alikuwa na usiku wenye mchanganyiko wa matukio, akifunga mabao mawili yaliyoiweka Bayern kifua mbele kabla hajatolewa uwanjani kwa kadi nyekundu muda mfupi kabla ya mapumziko, kufuatia rafu ya nyuma kwa Achraf Hakimi ambayo ilimwacha beki huyo wa PSG akiwa na maumivu makali ya kifundo cha mguu, akatolewa uwanjani huku akilia.

Katika kipindi cha kwanza kilichojaa vurugu kwenye Uwanja wa Parc des Princes, kikosi cha Vincent Kompany kilionyesha ujasiri na hamasa kubwa kwa kucheza soka la kushambulia tangu mwanzo, jambo lililowazawadia bao la mapema dakika ya 4 kupitia Díaz.

Ousmane Dembélé alidhani ameisawazishia PSG katikati ya kipindi cha kwanza baada ya kupachika mpira wavuni kwa kifua, lakini bao hilo lilifutwa kwa ofsaidi.

Mshindi huyo wa Ballon d’Or alilazimika kutoka uwanjani muda mfupi baadaye kutokana na maumivu ya misuli ya mguu.

Bayern waliendelea kuishambulia PSG na walikaribia kuongeza bao kufuatia shuti la Serge Gnabry kugonga nguzo moja na kurudi kugonga nyingine.

Díaz alipachika bao lake la pili dakika ya 32 baada ya kumnyang’anya mpira Marquinhos na kumalizia kwa ustadi mkubwa.

Hata hivyo, winga huyo wa Colombia alipewa kadi nyekundu kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika baada ya VAR kubadilisha onyo la awali (kadi ya njano) kuwa nyekundu kwa sababu ya ukali wa rafu yake kwa Hakimi.

Kipindi cha pili PSG walishambulia kwa nguvu wakitafuta njia ya kusawazisha, lakini waligonga mwamba kila walipojaribu, huku Manuel Neuer akiwa imara langoni mwa Bayern.

Dakika 16 kabla ya mchezo kumalizika, João Neves aliipatia PSG tumaini baada ya kufunga kwa bicycle kick iliyomshinda Neuer.

Bao hilo liliwapa nguvu wapinzani, lakini Neuer alifanya kazi ya ziada kwa kuokoa mashuti kadhaa kutoka kwa Neves, Warren Zaïre-Emery, na Vitinha.

Licha ya jitihada hizo, PSG imepoteza kwa mara ya kwanza msimu huu katika Ligi ya Mabingwa.