Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Abramovich kukomalia pesa za mauzo ya Chelsea

Muktasari:

  • Mwaka 2022, bilionea huyo aliuza klabu hiyo ya Ligi Kuu England baada ya kuanza kwa vita nchini Ukraine na kutokana na uhusiano wake na Rais wa Russia, Vladimir Putin. Wakati huo Abramovich alisema aliamua kuuza klabu hiyo kwa sababu ilikuwa kwa maslahi bora ya klabu.

LONDON, ENGLAND: JOPO la wanasheria wa bilionea Roman Abramovich wako tayari kupambana na serikali ya Uingereza kuhusu haki ya kutumia Pauni 2.35 bilioni zilizopatikana kwenye mauzo ya Chelsea, fedha ambazo bado hazijatumika.

Mwaka 2022, bilionea huyo aliuza klabu hiyo ya Ligi Kuu England baada ya kuanza kwa vita nchini Ukraine na kutokana na uhusiano wake na Rais wa Russia, Vladimir Putin. Wakati huo Abramovich alisema aliamua kuuza klabu hiyo kwa sababu ilikuwa kwa maslahi bora ya klabu.

Fedha zilizopatikana kutokana na mauzo hayo bado zimefungiwa katika akaunti ya benki ya kampuni ya Abramovich, Fordstam Ltd, kutokana na mgogoro unaoendelea kuhusu jinsi zitakavyotumika kusaidia waathirika wa vita vya Ukraine.

Barua kutoka kwa kampuni ya sheria inayomwakilisha tajiri Abramovich inaeleza kuwa bado amejitolea kikamilifu kutumia fedha hizo kwa madhumuni ya misaada, lakini vikwazo vilivyowekwa na serikali vinaathiri namna fedha hizo zinavyoweza kutumika.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer aliweka tarehe ya mwisho ya Machi 17 kwa Abramovich kutoa fedha zote Pauni 2.35 bilioni ili ziende kwa taasisi mpya ya kusaidia Ukraine, huku hatua za kisheria zikitarajiwa kuchukuliwa kama hatatekeleza hilo.

Hata hivyo, Abramovich anataka fedha hizo zitumike kusaidia waathirika wote wa vita na yuko tayari kupambana mahakamani kuhusu suala hilo.

Gazeti la The Times limeona barua kutoka kwa wanasheria wa Abramovich ambayo inasema: “Kwa kushangaza, serikali ya Uingereza inaonekana kuchukulia mchango huu uliopendekezwa kama aina ya adhabu dhidi ya Bw. Abramovich. Hii si sahihi kabisa. Ni muhimu kusisitiza fedha hizi, ingawa kwa sasa zimefungiwa bado ni mali ya Fordstam Limited, ambayo inamilikiwa kikamilifu na Bw. Abramovich.

“Iwapo serikali ya Uingereza inaamini ina msingi wa kisheria wa kuzichukua fedha hizi, basi inaweza kuanzisha rasmi mchakato wa kuzitaifisha, jambo ambalo litapingwa mahakamani.”