Prime
Abramovich kajichimbia Uturuki, kodi Sh122 milioni

ISTANBUL, UTURUKI. NDO hivyo, baada ya ukimya wa muda mrefu kila mtu akijiuliza yuko wapi tajiri na mmiliki wa zamani wa Chelsea Roman Abramovich imegundulika kwamba bwanyenye huyu yupo zake huko nchini Uturuki katika Jiji la Instanbul ambapo amepanga na analipa zaidi ya shilingi milioni 122 kwa mwezi kama kodi.
Abramovic kwa sasa anaishi kwenye fukwe ambayo na ni ngumu sana kusogelea makazi yake kutokana na ulinzi mkubwa uliopo hali inayosababisha hata jirani zake kutokukutana naye.
Fukwe hiyo ipo kwenye maeneo ya Anadolu Hisari katika Jiji la Istanbul mahali ambapo wanaishi matajiri wengi nchini Uturuki.
Mbele ya nyumba anayoshi anapata kuona mandhari nzuri ya bahari, vilevile sehemu hiyo inaunganisha bahari mbili ile bahari nyeusi na ile ya Marmara.
Nyumba hiyo ambayo kwa sasa inamilikiwa na Ahmet Okumus ambaye ni mfanya biashara maarufu nchini Uturuki kwa mwezi gharama yake ya kupanga ni Dola 50,000 ambayo ni zaidi ya shilingi 122 za kibongo.
Hata hivyo nyumba hiyo haionekani kuwa inakaliwa na mtu kwani ipo kimya sana kwani hata taa haziwashi lakini miezi sita iliyopita wachunguzi wa mambo walituma ndege isiyokuwa na rubani (Drone) kwenda kuhunguza na wakabahatika kumuona Roman hiyo ilikuwa ni desemba mwaka huu.
Mjengo huu anaokaa bilionea huyu ulijengwa mwaka 1393 hadi 1394 kama sehemu ya makazi ya utawala wa Ottoman Empire Kwa mujibu wa klabu ya kampuni za udalali nchini Uturuki, mmiliki wa mjengo huo Ahmet Okumus aliinunua mwaka jana kwa Pauni 20 milioni ambazo ni zaidi ya bilioni 40 za Kitanzania.
Abramovic aliondoka England na kuiuza Chelsea kwa Toddy Boehly kwa Pauni 4.5 bilioni baada ya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na serikali ya nchi hiyo akishtumiwa kwamba anamsaidia rais wa Urusi Vladimir Putin kwenye
kuivamia Ukraine.
Kuondoka kwake kulisitisha utawala wake wa miaka 19 kuimiliki timu hiyo ambayo chini yake ilipata mafanikio mbali mbali ndani na nje ya England.
Abramovic ambaye utajiri wake unatokana na kumiliki makampuni ya uuzaji wa mafuta ya petroli na Dizeli alikuwa akihusishwa kuwa kwenye mpango wa kutaka kuinunua moja ya timu nchini Uturuki lakini jambo hilo halijatimia hadi sasa.