Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Viktor Gyokeres apewa muda

GYOKERES Pict

Muktasari:

  • Gyokeres, mwenye umri wa miaka 27, yupo katika mvutano na rais wa Sporting, Frederico Varandas, kuhusu ada yake ya uhamisho ambapo ameshawaambia viongozi wa timu hiyo kuwa hatorudi klabuni kufanya mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya Jumanne ya wiki hii kama wataendelea kukiuka makubaliano yao.

LISBON, URENO: STRAIKA wa Sporting Lisbon na timu ya taifa ya Sweden, Viktor Gyokeres, anayewindwa na Manchester United, Liverpool na Arsenal, amepewa muda wa ziada wa mapumziko na na timu yake wakati suala lake la uhamisho likiendelea kutatuliwa.

Gyokeres, mwenye umri wa miaka 27, yupo katika mvutano na rais wa Sporting, Frederico Varandas, kuhusu ada yake ya uhamisho ambapo ameshawaambia viongozi wa timu hiyo kuwa hatorudi klabuni kufanya mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya Jumanne ya wiki hii kama wataendelea kukiuka makubaliano yao.

Hata hivyo, licha ya wachezaji wote kutakiwa kurejea kuanza mazoezi kesho, Sporting imempa Gyokeres ruhusa ya kurejea Julai 7, jambo linalozipa timu za Ligi Kuu England nafasi ya kujaribu kumsajili.

Gyokeres anadai kuwa Sporting wamekiuka makubaliano yao ya kumuuza kwa bei ya chini zaidi ya kifungu chake kinachotaka aachiliwe ikiwa timu inayomhitaji italipa pauni 85 milioni.

Inaelezwa katika dirisha lililopita la majira ya baridi staa huyu pamoja na mabosi wa Sporting walikubaliana kwamba anaweza kuondoka kwa kiasi kisichozidi pauni 50 milioni ikiwa sehemu ya kumshawishi asiondoke katikati ya msimu licha ya kuwepo kwa timu zilizohitaji kumsajili kwa wakati huo.

Kwa sasa Sporting inasisitiza kwamba yeyote anayetaka huduma za Gyokeres atalazimika kulipa angalau pauni 65  milioni.

Arsenal, inatajwa kuwa moja ya timu zilizowasilisha mapema ofa ya kumsajili staa huyu lakini ilikuwa ni pungufu ya pauni 10 milioni ya kiasi ambacho Sporting inakihitaji.

Gyokeres anatajwa kutaka sana kwenda Arsenal ambayo pia inadaiwa kumhitaji sana kwa sababu imeshindwa kufikia mwafaka na mpango wao wa kumsajili mshambuliaji wa RB Leipzig, Benjamin Sesko, mwenye umri wa miaka 22.

RB Leipzig bado haijapokea ofa yoyote rasmi kwa Sesko, ambaye alifunga mabao 21 katika mechi 45 za mashindano yote msimu uliopita.