Tottenham yaicharukia bodi Ligi Kuu England

Tottenham yaicharukia bodi Ligi Kuu England

LONDON, ENGLAND. KLABU ya Tottenham inataka majibu ya Bodi ya Ligi Kuu England kutokana na uamuzi wao ya kuifuta mechi yao dhidi ya Arsenal ambayo ilikuwa ichezwe jana lakini haukufanyika.

Mechi hiyo ilipigwa ‘stop’ baada ya Mikel Arteta kuomba mchezo huo kuahirishwa kutokana na kikosi chake kukumbwa na lundo la wachezaji majeruhi na wengine kuugua maradhi ya kawaida.

Maswali mengi watu wamejiuliza kuhusu maamuzi hayo huku Tottenham ikiweka wazi haikuwa na sababu ya mchezo huo kutochezwa wakiamini kuwa ni ujanja tu ambao Arsenal imeufanya.

Aidha Bodi ya Ligi Kuu England imetolea ufafanuzi kuhusu uamuzi huo baada ya uthibitisho na kuridhia matakwa ya Arsenal.

“Tumeangalia timu ya Arsenal ina wachezaji 13, pamoja kipa mmoja, maamuzi haya pia ni matokeo ya janga la corona , majeruhi ya wachezaji pamoja na wengine ambao wapo katika majukumu yao timu ya taifa kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) yanayoendelea Cameroon.

Licha ya kauli hiyo ya Bodi ya Ligi Kuu England, Tottenham haikupendezwa kabisa na maamuzi hayo na wakaandika maelezo kupita tovuti yao maalumu.

“Tunasikita kutangaza kwamba mechi yetu dhidi ya Arsenal haitachezwa hii ni kutokana na maombi ya wenzetu ambao wanakabiliwa na matatizo binafsi ya wachezaji, tumeshangazwa sana maamuzi haya ya bodi.”