Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‎ Madrid yaanza kujipanga kwa Ruben Neves

Muktasari:

  • Neves, aliyewahi kucheza Ligi Kuu England akiwa na Wolves, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na hadi sasa amekataa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika kikosi hicho ikielezwa anataka kuondoka na kurudi barani Ulaya kwa ajili ya kucheza soka la kiushindani.

REAL Madrid ni miongoni mwa klabu zinazotajwa kufikiria kutaka kumsajili kiungo wa Al-Hilal na timu ya taifa ya Ureno, Ruben Neves, mwenye umri wa miaka 28.

Neves, aliyewahi kucheza Ligi Kuu England akiwa na Wolves, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na hadi sasa amekataa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika kikosi hicho ikielezwa anataka kuondoka na kurudi barani Ulaya kwa ajili ya kucheza soka la kiushindani.

Al‑Hilal inadaiwa huenda ikahitaji takribani Pauni 20 milioni ili kumuuza staa huyu Januari ili kuzuia asiondoke bure dirisha la majira ya kiangazi.

Kwa sasa anakunja jumla ya Pauni 350,000 kwa wiki akiwa na kikosi cha Al-Hilal aliyojiunga nayo mwaka 2023 kwa ada ya takribani Pauni 47 milioni.

Mbali ya Madrid, kule England, Chelsea na Manchester United ni miongoni mwa timu ambazo zinahitaji saini ya staa huyu.


Antoine Semenyo

WINGA wa Bournemouth na timu ya taifa ya Ghana, Antoine Semenyo, mwenye umri wa miaka 25, bado anaendelea kuwapiganisha vigogo wanne wa Ligi Kuu England ambao ni Manchester United, Manchester City, Liverpool na Tottenham Hotspur. Klabu hizo tayari zimefungua mazungumzo ya awali kuhusu uwezekano wa kumsajili kwa dau linalokadiriwa kufikia Pauni 65  milioni. Man United inaamini Semenyo anaweza kuimarisha upande wao wa kushoto wa safu ya ushambuliaji. Mkataba wa Semenyo na Bournemouth unamalizika mwaka 2030.


Brennan Johnson

BOURNEMOUTH inamwangalia winga wa Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Wales, Brennan Johnson, mwenye umri wa miaka 24, kama mbadala wao ikiwa itamuuza Antoine Semenyo katika dirisha lijalo la Januari. Johnson alijiunga na Spurs mwaka 2023 akitokea Nottingham Forest, lakini hajapata nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo hali inayofanya Tottenham kuwa tayari kusikiliza ofa ili kumuuza. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.

Marcus Rashford

BARCELONA inatajwa kuwa karibu zaidi kumsainisha mkataba wa moja kwa moja mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 28, dirisha lijalo.

Katika makubaliano yao ya mkopo, Barca inaruhusiwa kumsainisha Rashford mkataba wa moja kwa moja ikiwa italipa Pauni 26 milioni tu. Rashford, anaonekana kurejesha kiwango chake akiwa na Barca kwa msimu huu. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Armand Lauriente

MSHAMBULIAJI wa Sassuolo naUfaransa, Armand Laurienti, mwenye umri wa miaka 27, yuko tayari anataka kulazimisha kuondoka katika klabu hiyo katika dirisha la usajili la Januari. Lauriente amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu na Sunderland na inaelezwa anatamani sana kwenda England akiamini soka lake litakuwa zaidi. Sassuolo bado haijatoa taarifa yoyote ikiwa itakuwa tayari kumuuza au laa.


Thiago Silva

AC MILAN inapanga kumsajili  beki mkongwe raia wa Brazil, Thiago Silva, mwenye umri wa miaka 41, dirisha la usajili la majira ya baridi. Silva, ambaye aliwahi kucheza timu hiyo kati ya mwaka 2009 na 2012, kwa sasa yuko huru baada ya kuvunja mkataba wake na Fluminense kwa makubaliano ya pande zote mbili. Milan inaamini uzoefu wake mkubwa unaweza kusaidia kuimarisha safu yao ya  ulinzi.


Lewis Dunk

KAPTENI  wa Brighton  na beki wa kati wa timu ya taifa ya England, Lewis Dunk, mwenye umri wa miaka 34, ameongeza mkataba wa mwaka mmoja. Mkataba huo utamwezesha Dunk kubakia katika viunga vya Amex Stadium hadi mwaka 2027, akiendelea kuwa nguzo muhimu ya safu ya ulinzi wa kikosi hicho. Dunk amekuwa mchezaji mwaminifu wa Brighton kwa zaidi ya miaka 10 sasa.



Denzel Dumfries

MANCHESTER United, Newcastle United na Aston Villa zote zimeonyesha nia ya kumsajili beki wa pembeni Inter Milan na timu ya taifa ya Uholanzi, Denzel Dumfries, mwenye umri wa miaka 29. Dumfries amekuwa akionyesha kiwango cha juu Serie A na Ligi ya Mabingwa Ulaya, tangu msimu uliopita. Inter bado haijaeleza ikiwa itakuwa tayari kumwachia fundi huyo au laa. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.