Lacazette sasa azigonganisha Barcelona, Atletico, Milan

Friday November 26 2021
LACA PIC

MTIFUANO wa kuiwania saini ya straika wa Arsenal na Ufaransa, Alexandre Lacazette, 30, umeendelea kuwa mkubwa kwani hadi sasa Atletico Madrid, Barcelona, Newcastle na AC Milan zimeripotiwa kufuatilia kwa karibu uwezekano wa kuipata saini ya fundi huyo katika dirisha lijalo la majira ya baridi.

Lacazette ni miongoni mwa wachezaji ambao hawaonekani kuwa na nafasi chini ya Mikel Arteta hali inayosababisha hata yeye atamani kuondoka ili kutafuta timu itakayompa nafasi ya kucheza.

Tangu msimu huu uanze staa huyo amecheza mechi 10 za michuano yote na kufunga mabao matatu.

Katika wiki kadhaa zilizopita Arsenal ilisitisha mazungumzo na timu zote zilizokuwa zinaiwania saini ya mwamba huyu baada ya Arteta kutoa maelekezo kwamba shughuli zote za masuala ya usajili zisiendelee hadi dirisha litakapofunguliwa kwani linawavuruga.

Advertisement