Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

'Kibabu' kilichoweka rekodi tatu kali Afcon

Abidjan, Ivory Coast. Mchezaji nyota wa zamani wa Ligi Kuu England, Emilio Nsue ambaye alizitumikia klabu za Middlesbrough na Birmingham akicheza kama beki na pia winga, ameingia katika vitabu vya kumbukumbu za Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya kufunga ‘hat-trick’ wakati timu yake ya Equatorial Guinea ikiichakaza Guinea-Bissau 4-2.

Lakini kitakachokushangaza ni nini? Huyu jamaa ni 'babu' mwenye umri wa miaka 34 na siku 110, ambaye sasa anaitumikia klabu ya Intercity ya Ligi Daraja la Tatu nchini Hispania, na ndiye nahodha wa timu yake ya taifa na anayeongoza safu ya ushambuliaji.

Utashangaa zaidi kwamba Nsue sio kibabu tu aliyefunga ‘hat-trick’ katika fainali za Afcon, lakini bao zake alizowachapa guinea Bissau zimekuja baada ya kupita miaka 15 na siku 362 tangu jamaa mmoja aliyeitwa Soufiane Alloudi alipofanya hivyo akiichezea Morocco alipoifumua Namibia, Januari 2008..

Nsue sasa ameingia katika orodha ya wababe wachache waliowahi kufanya hivyo akiwamo Samuel Eto’o wa Cameroon, Hossam Hassan wa Misri na Benni McCarthy wa Afrika Kusini.

Balaa la 'babu' huyu alijaishia katika mabao hayo tu aliyofunga kwenye Afcon za mwaka huu, lakini pia unaambiwa katika umri wake miaka 34 na siku 110, Nsue ndiye mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kwa wachezaji wa kizazi cha sasa aliyefunga bao katika fainali hizi akifuata nyayo za jamaa aliyefahamika kwa jina la Ima Andriatsima (miaka 35 na siku 34) alipoichezea Madagascar DR Congo Julai 2019.

Nsue ambaye pia aliwahi kuzitumikia klabu za Real Sociedad na Mallorca za Hispania, anaongoza katika mbio za ufungaji bora wa fainali hizo za Ivory Coast akifuatiwa na wachezaji wenye mabao mawili mawili, Mohamed Kudus wa Ghana aliyepiga mabao mawili juzi dhidi ya Misri, Lamine Camara wa Senegal na Mostafa Mohamed wa Misri.

Timu yake ya Equatorial Guinea imemshangaza kila mtu ikiongoza Kundi A la Afcon linaloijumuisha timu mwenyeji wa fainali hizo, Ivory Coast na Nigeria, ikiwa na pointi nne kileleni baada ya mechi mbili, lakini imelingana na Nigeria iliyo katika nafasi ya pili ikiwa pointi nne pia, huku wenyeji wakiwa na pointi tatu katika nafasi ya tatu. Guinea Bissau iko mkiani ikiwa haina pointi. Equatorial Guinea ilianza kwa kulazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Nigeria na itamaliza kwa kuwavaa wenyeji Ivory Coast keshokutwa Jumatatu.