Brighton yaikana Chelsea dili la Cucurella

Brighton yaikana Chelsea dili la Cucurella

LONDON ENGLAND. KLABU ya Chelsea iko mbioni kuinasa saini ya beki Marc Cucurella kwa kitita cha Pauni 52.5 milioni, licha ya Brighton kukana taarifa hizo usiku wa kuamkia jana na kuzua gumzo mtandaoni.

Brighton imesisitiza haijafikia makubaliano na klabu yoyote, kuhusu uhamisho wa beki huyo, aliyewaniwa na Man City pia, Aidha wakati Brighton ikipinga kuhusu taarifa hiyo, huenda Cucurella akapimwa vipimo vya afya, hadi tunaingia mtamboni na atasaini mkataba wa mikaka sita kwa mujibu wa ripoti.

Imeaminika Cucurellla amefosi uhamisho wake wa kujiunga na Chelsea baada ya kuomba ruhusa ya kuondoka tangu Man City ilipoonyesha nia ya kumsajili beki huyo na ilikuwa tayari kutoa Pauni 40 milioni, lakini ofa hiyo ikaigwa chini.

Wakati huohuo Klabu ya Brighton imeweka wazi kuhusu taarifa ya Cucurella kuwa yupo mbioni kujiunga na Chelsea, kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter ikisisitiza, haijafikia makubaliano na klabu yoyote.

“Kutokana na taarifa zilizosambaa mtandaoni kuhusu Cucurella, tunathibitisa hatujafikia makubaliano kuhusu uhamisho huu na klabu yoyote, kwaajili ya kumuuza Cucurella,”

Lakini kwa upande wa Cucurella amekubali kujiunga na Chelsea na anachosuburi ni ruhusa tu kutoka Brighton baada ya mambo kuwekwa sawa pande zote.

Man City ilivutiwa na beki huyo na endapo ingefanikiwa kuinasa saini yake, angekuwa mbadala wa Oleksandr Zinchenko aliyetimkia Arsenal. Cucurella amecheza jumla ya mechi 35 msimu uliyopita na kufunga bao moja tu.