Big Six yajitoa Super League

LONDON, ENGLAND. KLABU sita za Ligi Kuu England zilizokuwa zikihusishwa kukubali  kushiriki michuano mipya ya European Super League (ESL) zimefikia maamuzi ya kujitoa.

Manchester City ndio waliokuwa wa kwanza  kujitoa baada ya Chelsea kuashiria nia yao ya kufanya hivyo kwa kuandaa nyaraka za kujiondoa.

Klabu nyingine zilizofuata nyayo za Manchester City na Chelsea kwa England, zilikuwa Arsenal, Liverpool, Manchester United na Tottenham.

Wakati hayo yakitokea, inaelezwa kwamba miamba ya soka la Italia, Inter Milan na yenyewe inajiandaa kujiondoa kwenye mpango huo wa mashindano hayo.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha BBC huko nchini England imethibitika kwamba Mabosi klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Italia 'Serie A' wanaweza kutangaza muda wowote juu ya uamuzi huo wa kujiondoa kama ilivyokuwa kwa klabu za Kiingereza.