Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakenya walivyotawala mashindano ya gofu Arusha

GOFU Pict

Muktasari:

  • Mashindano hayo yaliyoshirikisha wachezaji zaidi ya 150 upande wa wachezaji wa kulipwa, Njoroge Kibugu aliibuka mshindi wa kwanza kwa mikwaju 289.

WACHEZAJI wa kulipwa na ridhaa wa gofu kutoka Kenya wametawala mashindano ya wazi yaliyofanyika wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Kiligolf, Arusha.

Mashindano hayo yaliyoshirikisha wachezaji zaidi ya 150 upande wa wachezaji wa kulipwa, Njoroge Kibugu aliibuka mshindi wa kwanza kwa mikwaju 289.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Greg Snow wa Kenya kwa mikwaju 300 ambapo Robinson Owiti pia wa Kenya alimaliza wa tatu kwa mikwaju 303.

Mtanzania Nuru Mollel alimaliza wa nne kwa mikwaju 305 akifuatiwa na Mtanzania mwingine Isaac Wanyeche katika nafasi ya tano kwa mikwaju 312.

Kwa upande wa wachezaji wa ridhaa, Wakenya waling’ara tena ambapo John Lejirma alishinda kwa mikwaju 292 akifuatiwa na Michael Karanga kwa mikwaju 297 na Mtanzania Isiaka Dunia akimaliza wa tatu kwa mikwaju 298.

Kwa upande wa wanawake, Madina Idd aliibuka wa kwanza kwa mikwaju 310, wapili Neema Olimi kwa mikwaju 315 katika mashindano hayo ya siku nne ya Stroke Play.

Mshindi wa kwanza kwa upande wa wachezaji wa kulipwa alizawadiwa Sh8.2 milioni ambapo mshindi wa kwanza kwa upande wa wachezaji wa ridhaa aliwazawadiwa Sh2.5 milioni, huku wachezaji 22 wakizawadiwa fedha taslimu.

GOF 01

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Vodacom, David Tarimo aliwapongeza washindi kwa kufanya vyema katika mashindano hayo.

“Mashindano yalikuwa ya kusisimua na sisi tunajivunia kuyadhamini. Tumeshuhudia ushindani wa kusisimua, vipaji vya kustaajibsha na shauku kubwa kwa michezo,” alisema.

Tarimo alisema kuwa mchezo wa gofu unaakisi maadili ya mipango yao ikiwa pamoja na nidhamu na lengo kubwa la kuwekeza katika mchezo huo ni kuinua vipaji vya ndani, kukuza ushirikiano wa kikanda, na kuiweka Tanzania kama kituo cha matukio ya michezo ya kiwango cha kimataifa.

“Mwaka huu tumeunganisha teknolojia ya kisasa katika mashindano haya kuanzia taarifa za matokeo ya moja kwa moja hadi uzoefu wa mashabiki unaoendeshwa na mtandao wetu.”

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU), Gilman Kasiga aliwapongeza wadhamini kufanikisha mashindano ya mchezo huo kwa mwaka wa tatu mfululizo.

“Tunajivunia kushirikiana na Vodacom kwa mashindano ya mwaka huu. Dhamira yao ya ubora na ubunifu imepandisha kiwango cha mashindano ya gofu nchini,” alisema Kasiga.

Alisema kuwa mashindano ya mwaka huu yameonyesha vipaji vya hali ya juu na jinsi ya  ushirikiano wa kimkakati unavyoweza kukuza michezo na kuhamasisha jamii.