Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Raila ailiza familia ya michezo

Muktasari:

  • Tawi la Kaunti ya Mombasa la Shirikisho la Soka nchini (FKF) lilijumuika na Wakenya wengine kuomboleza kifo cha Odinga huku likitangaza rasmi kusimamishwa kwa mechi za ligi zote kwa kipindi chote cha maombolezi.

WASHIKA dau wa michezo mbalimbali wa Kanda ya Pwani ya Kenya wametuma rambirambi zao kueleza masikitiko makubwa juu ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu, Raila Amolo Odinga.

Tawi la Kaunti ya Mombasa la Shirikisho la Soka nchini (FKF) lilijumuika na Wakenya wengine kuomboleza kifo cha Odinga huku likitangaza rasmi kusimamishwa kwa mechi za ligi zote kwa kipindi chote cha maombolezi.

Taarifa ya tawi hilo ilisema: “Tunajumuika na dunia yote kuomboleza na kuthibitisha heshima zetu kipindi hiki cha maombolezi ya kifo cha Raila ambaye amekuwa shabiki mkubwa wa soka na kiongozi aliyependa na kujitolea kuhakikisha Wakenya wanaishi kwa umoja.”

Naye Mwenyekiti wa FKF wa Kaunti ya Kilifi, Dickson Angore amesema kutokana na kipindi cha maobolezi cha kifo cha Odinga, mechi za ligi zote za shirikisho hilo zimeahirishwa hadi kipindi cha maombolezi cha siku saba kitakapomalizika.

“Kwa niaba ya wachezaji, maafisa wa klabu, marefarii, viongozi wa FKF wa tawi letu, tunatuma risala za rambirambi kwa familia ya marehemu tukimuombea Mungu amuweke mahali pema penye wema,” ikasema risala ya Angore.

Afisa Mkuu Mtendaji wa FKF Kaunti ya Kwale, Shaban Mwero amesema wamehuzunishwa mno na kifo cha Odinga ambaye alimtaja kama mpenda maendeleo ya michezo mbalimbali kwa vijana.

“Kutokana na huzuni tuliyonayo, tunatuma risala za pole nyingi kwa familia yake pamoja na washiriki wake wote katika nyanja za kisiasa na hata michezo,” akasema Mwero.

Ni jambo la dhahiri kuwa marehemu Odinga alikuwa shabiki sugu wa timu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Arsenal na kutokana na ushabiki wake wa timu hiyo, amethibitisha kuwa ni mpenda soka nambari moja nchini Kenya.