Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nairobi United yaandika historia, yaitupa nje Etoile du Sahel ikitinga makundi Afrika

NAIROBI Pict

Muktasari:

  • Naiboys ilipata ushindi huo wa penalti 7-6 baada ya dakika 90 mechi ya marudiano iliyochezwa usiku wa jana huko Tunisia kuisha kwa kipigo cha mabao 2-0 na kufanya matokeo ya jumla kuwa sare ya 2-2 kwani wiki iliyopita timu hiyo ya Kenya ilishinda pia idadi ka hiyo jiji Nairobi. 

KLABU ya Ligi Kuu ya Kenya, Nairobi United, imeandika historia baada ya kufuzu kwa mara ya kwanza kabisa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ikiing'oa kwa penalti mabingwa wa zamani wa CAF, Etoile du Sahel ya Tunisia.

Naiboys ilipata ushindi huo wa penalti 7-6 baada ya dakika 90 mechi ya marudiano iliyochezwa usiku wa jana huko Tunisia kuisha kwa kipigo cha mabao 2-0 na kufanya matokeo ya jumla kuwa sare ya 2-2 kwani wiki iliyopita timu hiyo ya Kenya ilishinda pia idadi ka hiyo jiji Nairobi. 

Katika pambano hilo la jana lililochezwa kwenye Uwanja wa Stade Olympique de Sousse  wenyeji walionekana dhahiri kudhamiria kupindua meza mbele ya Naiboys licha ya dakika 45 za kwanza kumalizika kwa suluhu.

 Rayan Anen aliifungia wenyeji bao mwanzoni mwa kipindi cha pili, kabla ya Ben Maazouz kufunga kwa kichwa dakika za majeruhi na kufanya matokeo kuwa 2-2, hivyo kupeleka pambano hilo katika mikwaju ya penalti.

Kipa wa United, Kevin Oduor, aligeuka shujaa baada ya kuokoa penalti ya saba ya Etoile, kisha yeye mwenyewe kufunga mkwaju wa ushindi uliowapa timu hiyo tiketi ya kihistoria ya kucheza hatua ya makundi ya michuano ya CAF kwa mara ya kwanza.

Etoile ilianza mchezo kwa kasi huku mshambuliaji Moussa Senghor akipiga shuti la mbali lililodakwa vyema na Oduor. Fursa nyingine ilimkuta Senghor tena, lakini akapiga kichwa nje baada ya beki Alphonse Omija kufanya kazi nzuri upande wa kulia.

Ovella Ochieng, aliyefunga katika mechi ya kwanza, alijaribu shuti la kwanza kwa upande wa United, lakini halikumtatiza kipa Sabri Ben Hassen.

Etoile ilikaribia tena kufunga dakika ya 24 baada ya kipa Ben Hassen kutoa mpira mrefu uliomkuta Senghor, lakini kabla hajapiga shuti, Kevin Otiende aliokoa kwa ustadi mkubwa.

Dakika ya 30, Etoile ilipata mpira wa adhabu nje ya eneo hatari, lakini Salaheddine Ghedamsi alishindwa kulivuka ukuta wa United. Nafasi hiyo iliyopotea iliwapa wachezaji wa United afueni kubwa walipoendelea kujilinda kwa nguvu.

Kipindi cha pili kilianza kwa Etoile kushambulia kwa kasi na dakika ya 50 walipata bao la kwanza kupitia kwa Rayan Anen, aliyepiga shuti kali kwa mguu wa kulia na kumtungua Oduor.

Wenyeji walipata bao la pili dakika za majeruhi, lakini Wakenya walishikilia hadi mikwaju ya penalti, ambapo walibeba ushindi.

Nairobi United ilifika hatua hii baada ya kutwaa kombe la FKF msimu uliopita, siku ya mwisho ya ligi.  

Ikiwa timu iliyopandishwa daraja na ilishangaza wengi kwa kuwafunga mabingwa wa kihistoria Gor Mahia (K’Ogalo) kwa mabao 2-1 na kuwa timu ya pili katika historia ya Kenya baada ya Mathare United kushinda kombe hilo ikiwa wapya katika Ligi Kuu.

Katika raundi ya kwanza ya kufuzu makundi ya CAF msimu huu, United ipangwa na NEC FC ya Uganda ambayo iliibana kwao jijini Kampala katika mechi ya kwanza iliyosha kwa sare ya 2-2 na ziliporudiana jijini Nairobi ikimalizika kwa sare ya 1-1, matokeo yaliyoiwezesha kusonga mbele kwa faida ya bao la ugenini.


United sasa inakuwa timu pekee ya Kenya katika hatua ya makundi baada ya Kenya Police FC, mabingwa wa ligi, kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 4-1 na Al Hilal SC ya Sudan.

Timu nyingine zilizofuzu hatua ya makundi
Katika mechi nyingine za Kombe la Shirikisho zilizochezwa wikiendi hii  OC Safi ya Morocco ilifuzu licha ya kupoteza 2-1 dhidi ya Stade Tunisien huko Rades.

Awali ilitoka kushinda 2-0 nyumbani katika mechi ya kwanza, OC Safi imefuzu kwa jumla ya mabao 3-2 na kutinga hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika historia yao.


Timu nyingine zilizofanikiwa ni: Zesco United (Zambia) iliyotoka sare ya 1-1 na Jwaneng Galaxy ya Botswana na kushinda kwa jumla ya 5-4.

Royal Leopards (Eswatini)  iliyoitoa Maniema Union ya DR Congo kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1.

USM Alger (Algeria), iliibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Academie de FAD jijini Algiers na kufuzu kwa jumla ya 3-1.

Singida Black Stars na Azam FC za Tanzania nazo zilifuzu kwa mara ya kwanza makundi kwa kuzing'oa Flambeau de Center ya Burundi na KMKM ya Zanzibar zikiungana na Simba na Yanga zilizopenya katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuzitoa Nsingizini Hotspurs ya eSwatini na Silver Strikers ya Malawi na kuandika historia ya kuingiza timu nne kwa mpigo katika michuano ya CAF kwa mara ya kwanza.