Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha wa Gambia afichua sababu ya kuhamishia mechi Kenya

KOCHA Pict

Muktasari:

  • Gambia itapapatuana na Gaboni saa 10:00 jioni, huku msimamo wa Kundi F, ukionyesha Ivory Coast inaongoza kwa pointi 20, Gabon ikifuatia kwa pointi 19, huku Gambia iskishika nafasi ya tatu kwa pointi 10.

Kocha wa timu ya taifa ya The Gambia, Jonathan McKinstry, ametaja sababu za kuuchagua Uwanja wa Moi Kasarani kama uwanja wa nyumbani wa mechi muhimu ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Gabon itakayopigwa baadae leo Ijumaa.

Gambia itapapatuana na Gaboni saa 10:00 jioni, huku msimamo wa Kundi F, ukionyesha Ivory Coast inaongoza kwa pointi 20, Gabon ikifuatia kwa pointi 19, huku Gambia iskishika nafasi ya tatu kwa pointi 10.

Kocha McKinstry ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha Gor Mahia, amesema ubora wa Uwanja wa Moi uliopo Kasarani nchini Kenya ni sehemu ya sababu zilizomfanya kuuchagua kwa ajili ya mechi ya leo, lakini sababu kuu ni kutaka kupata urahisi wa safari ya kuelekea Mauritius kwa ajili ya mechi ya mwisho kufuzu Kombe la Dunia 2026 itakaopigwa wiki ijayo.

KOCH 01

Kocha huyo kutoka Ireland Kaskazini, ameongeza kuwa, uamuzi mwingine wa kucheza jijini Nairobi nchini Kenya ni suala ya kitaalamu na utulivu wa wachezaji kabla ya safari.

“Hatukutaka kucheza mechi zote mbili Mauritius kwa sababu huko kuna uwanja wa michezo wa majani ya bandia na hatutaki kucheza kwenye uwanja wa majani ya bandia,” McKinstry ameeleza.
 
“Hatujali kucheza kwenye majani ya bandia, lakini tunapopata nafasi ya kucheza kwenye majani halisi, tutachagua hilo kila wakati, na ndiyo maana tumerudi Kenya.”

KOCH 02

Kocha huyo amebainisha kuwa masuala ya usafiri na urahisi wa kusafiri yalichangia uamuzi wa kuchagua Nairobi kama makazi yao.

“Umbali kutoka Kenya kwenda Mauritius ni mfupi, na kuna safari za moja kwa moja kati ya nchi hizo mbili, hivyo ni busara kwetu kuweka makazi hapa,” aliongeza.

Katika hatua nyingine McKinstry, ambaye aliiongoza Gambia kushinda nyumbani mechi mbili mfululizo dhidi ya Burundi na Kenya mwezi uliopita, amesema wachezaji wake wamekuwa na furaha katika kipindi chote walichokaa Kenya, hali ambayo naye inamfurahisha kama mkuu wa benchi la ufundi la timu hiyo.

“Tulipokelewa kwa shangwe kubwa wakati tulipocheza hapa mara ya mwisho,” amesema.

KOCH 03

“Kucheza na Burundi hapa kulifanya kazi zaidi kwa sababu tulikuwa tunacheza na Kenya muda mfupi baadaye; ilitusaidia kuepuka safari zisizo za lazima na kudumisha mfululizo wa mechi.”

The Scorpions iliifunga Harambee Stars 3-1 Septemba 9, 2025 kabla ya kuifunga Burundi 2-0 siku nne baadaye. Katika mechi ya leo Ijumaa, McKinstry anatarajia upinzani mkali dhidi ya mpinzani anayeijua vyema timu yake.