Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha mpya Kenya Police atamba kufuata nyayo za Ndayiragije

KOCHA PIct
KOCHA PIct

Muktasari:

  • Stojanovic kutoka Serbia, alianza kazi yake kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Sofapaka jana Jumatano, Novemba 5, 2025, kwenye Uwanja wa Police Sacco.

Kocha mpya wa Kenya Police FC, Dusan Stojanovic, ametamba kufuata nyayo za mtangulizi wake, Etienne Ndayiragije, kwa kuhakikisha anatetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) msimu huu 2025-2026.

Stojanovic kutoka Serbia, alianza kazi yake kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Sofapaka jana Jumatano, Novemba 5, 2025, kwenye Uwanja wa Police Sacco.

Licha ya ushindi huo mdogo dhidi ya “Batoto ba Mungu,” Stojanovic anahisi mechi hiyo ilikuwa ngumu na ilikuwa na uwezo wa kupata mshindi kutoka upande wowote.

“Huu ni ushindi wa kwanza tu, lakini tunatafuta mwingine na hata zaidi. Tunatakiwa kusahau na kujipanga kwa mechi ijayo, lazima tuwe na mipango kuanzia hapa ili kufikia lengo la kutetea ubingwa wetu,” amesema Stojanovic.

Katika mechi hiyo, Stojanovic alitumia mbinu kali za ushambuliaji kipindi cha kwanza, na hatimaye Edward Omondi alifunga bao pekee katika dakika ya 40. Hata hivyo, alibadilisha mbinu kipindi cha pili, kwa kutengeneza safu kali ya ulinzi wa mstari wa chini (low-block defence).

“Ni kuhusu kusoma mechi na tulilazimika kubadilika kulingana na hali kuhakikisha tunadumisha ushindi wetu,” ameongeza kocha huyo.

Kocha huyo mwenye leseni ya UEFA, alitambulishwa rasmi Jumapili, Novemba 2, 2025 kwenye Uwanja wa Police Sacco, dakika chache baada ya kuangalia mechi ya Kenya Police dhidi ya Posta Rangers iliyomalizika kwa timu hizo kushindwa kufungana.

Stojanovic ameziba nafasi ya kocha Etienne Ndayiragije wa Burundi, aliyeondoka Oktoba 29, 2025, baada ya timu kushindwa kwa 4-1 dhidi ya Al Hilal katika raundi ya pili ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

KOCH 01
KOCH 01

“Tunapotetea ubingwa wetu wa ligi, tutaona mambo mengi sana, tutapata upinzani mkali sana kutoka kwa wapinzani wetu. Ligi ina timu nyingi zenye ushindani, na tunatarajia msimu mgumu wa 2025-2026,” amesema Stojanovic

Stojanovic, ambaye aliiongoza SC Villa ya Uganda kutwaa ubingwa wa ligi msimu wa 2023-2024, anatarajia kupambana na Gor Mahia, mabingwa wa rekodi ya mara 21, Jumapili, Novemba 9, 2025.