Gor Mahia yaanza kwa kipigo Ligi ya Mabingwa

Muktasari:

  • Mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Juba, Sudan ya Kusini ni muendelezo wa mabingwa hao wa Kenya kuwa na matokeo mabaya tangu ibebe taji la Ligi Kuu msimu uliopita.

BAO pekee lililofungwa dakika ya 64 na Mohammed Mussa wa Al Merrikh Benteu ya Sudan Kusini limeizamisha Gor Mahia ya Kenya katika mechi ya awali ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika jioni ya leo.

Mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Juba, Sudan ya Kusini ni muendelezo wa mabingwa hao wa Kenya kuwa na matokeo mabaya tangu ibebe taji la Ligi Kuu msimu uliopita.

Timu hiyo ilifanya vibaya katika michuano ya Kombe la Kagame 2024 iliyochezwa jijini Dar es Salaam mwezi uliopita.

Katika michuano ya Kagame Gor iling'olewa makundi kwa kufungwa mechi mbili dhidi ya Al Hilal ya Sudan na waliobeba ubingwa, Red Arrows ya Zambia na kuambulia sare y 1-1 dhidi ya ASAS ya Dijbouti.

Kwa kipigo hicho K'Ogalo sasa inahitaji ushindi kuanzia mabao 2-0  katika mechi ya marudiano Jumapili ijayo, jijini Nairobi ili itinge raundi ya pili.