Zungu aipiga kijembe Yanga mkutano Simba

Zungu aipiga kijembe Yanga mkutano Simba

Dar es Salaam. Mussa Azan Zungu ni kama ameipiga kijembe Yanga kwenye hotuba yake katika mkutano mkuu wa klabu ya Simba unaoendelea Dar es Salaam.

Zungu ambaye ni mgeni rasmi kwenye mkutano huo alitumia dakika 15 kuzungumza na moja ya vitu alivyozungumza ni kwamba baadhi ya watu wanaamini timu yao ndiyo ilishiriki kwenye uhuru wa Tanganyika.

"Hao hawajui historia ya nchi yetu, eti klabu yao imeshiriki kwenye uhuru," alitania Zungu huku akishangiliwa kwa nguvu na wanachama wa klabu hiyo.

Amesema viongozi waandaamizi wa Serikali akiwamo, aliyekuwa waziri mkuu, Rashid Mfaume Kawawa walikuwa ni wanachama wa klabu hiyo walioshirikiana ipasavyo na Mwalimu Nyerere.

"Wacha wajisifu tu, lakini Taifa letu ni moja na mwenyezi Mungu ni mmoja, lakini hawafahamu historia," amesema Zungu.

Katika hotuba yake pia ameupongeza uongozi wa klabu hiyo na Ofisa mtendaji mkuu, Barbara Gonzalez.

"Maneno yalikuwa mengi ulipoteuliwa kuwa CEO, lakini umeonyesha unaweza na sasa wewe ni CEO uliyekubuhu, usiogope vijembe na maneno hayo yapo tu," amesema.