Zaka awaita mashabiki Chamazi

Zaka awaita mashabiki Chamazi

OFISA habari wa Azam FC, Thabit Zakaria (Zaka Zakazi), amesema mashabiki wa timu hiyo wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Azam Complex Chamazi.

Zaka amesema kutokana na hali ilivyo na wingi wa mashabiki waliojitokeza kabla ya kufika saa 2:00 usiku muda wa mechi kuanza watakuwa wamejaza uwanja.

Amesema kutokana na muitikio wa mashabiki wa Azam na wale wa timu nyingine waliokwenda kujifunza ufanyaji wa matamasha kama hayo makubwa.

“Hii ni shughuli ya mashabiki wetu kwahiyo kila kitu kwa kiasi kikubwa kimefanywa na wao, tuwapongeze hadi sasa mambo ni mazuri tofauti na matarajio,” amesema Zaka na kuongeza;

“Mashabiki ambao watakuja hapa watapata budurani nyingi za kutosha kutoka kwa wachezaji wetu wapya na wale waliokuwepo msimu uliopita na huko kwenye mziki ndio balaa kabisa.

“Kama kuna shabiki yetu atashindwa kufika hapa basi naomba wafuatilie tamasha letu kupitia luninga watafurahi zaidi.”