Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yao arejea Yanga SC, Gamondi afunguka

BAADA ya kutokuonekana kwenye mchezo dhidi ya Azam kutokana na majeraha, beki kisiki wa Yanga Yao Kouassi pamoja na mshambuliaji Kennedy Musonda wamerejea.

Yanga inajiandaa kuvaana na Singida Big Stars mchezo utakaopigwa Ijumaa hii Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Musonda amekosekana kwenye mechi tatu mfululizo dhidi ya Ihefu FC, Geita Gold na Azam FC kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi amethibitisha ufiti wa mshambuliaji huyo.

Wakati Musonda akirejea beki kisiki wa timu hiyo aliyejiunga msimu huu na kuanza kwa kasi Yao amerudi kwenye uwanja wa mazoezi baada ya jeraha lake dogo alilolipata mazoezini kupona na hivyo ni uhuru wa kocha kama ataamua kumtumia kwenye mchezo dhidi ya Singida au hapana. Kurudi kwa mastaa hao kunatoa wigo mpana kwa Gamondi kupangilia kikosi chake kuelekea mchezo wao dhidi ya Singida Big Stars Ijumaa.

Gamondi alisema anakiandaa kikosi chake kiwe kamili baada ya wachezaji wake wote kuwa katika hali nzuri; “Musonda kutokutumika kwenye mechi tatu mfululizo kunatokana na kusumbuliwa na jeraha la enka amepata nafuu suala la kumtumika litategemea na namna atakavyoamka siku ya mchezo;

“Tayari ameshaanza mazoezi tangu Jumapili iliyopita lakini sikuona sababu za kumtumia dhidi ya Azam FC kutokana na kuhofia kumpa presha na akapata shida nyingine nikampa mapumziko.” alisema.

Akimzungumzia Yao, alisema pia alikuwa na shida ya enka aliumia kwenye mazoezini amerejea kikosini na anaendelea vizuri .

“Kila mchezaji ndani ya Yanga ana umuhimu wake hivyo kurudi kwa wachezaji hao ambao wana mchango mkubwa ndani ya timu katika mechi sita tulizocheza naamini wataongeza nguvu na kasi ya kufikia malengo;

“Yao amehusika kwenye mabao mengi ya timu pia Musonda amefunga hivyo kurudi kwao wataongeza nguvu na kasi kutokana na kuwa na nguvu walizozitunza baada ya kukosekana kwenye michezo kadhaa.” alisema Gamondi.

Musonda kwenye mechi sita walizocheza Yanga yeye amecheza tatu, amefunga bao moja huku Yao akifunga bao moja na ametoa pasi tatu.