Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yazitaka rekodi Ligi ya Mabingwa

Kesho katika uwanja wa Azam Complex utachezwa mchezo wa ligi ya Mabingwa barani Afrika mchezo utakao wakutanisha mabingwa wa ligi ya Djibouti ASAS na mabingwa wa ligi ya Tanzania Yanga.

Kuelekea mchezo huo makocha pamoja na manahodha wamezungumza na waandishi wa habari wakielezea mipango yao.

Miguel Gamondi kocha wa Yanga amesema, wamejipanga vizuri kuelekea mchezo huo licha ya kutokujua uimara na udhaifu wa wapinzani wao.

Amesema yeye Ni Kocha mpya na anatamani kuweka historia yake mpya ikiwa Yanga inahistoria ya kutoingia makundi ya ligi ya Mabingwa kwa miaka ya hivi karibuni.

"Tumejipanga vizuri, hatumfahamu mpinzani kiundani lakini tumejipanga kufanya vizuri na kuandika historia mpya".

Nickson Kibabage (Yanga) ambaye aliambatana na kocha amesema kwa upande wa wachezaji wako vizuri, ASAS wanatakiwa kujifunza kuipitia wao,na yeye kama mchezaji anatamani kuandika historia mpya ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki mashindano hayo.

"Sisi kama wachezaji tumejiandaa vizuri tumesikiliza maelekezo ya mwalimu tunatamani ASAS wajifunze kupitia kwetu".

Kwa upande wao timu ya ASAS kupitia kwa kocha msaidizi Mohamed Kader Daher Ahmed amesema wao wamejianda vizuri licha ya kuwa timu ndogo ukilinganishana na Yanga, amekiri hali ya hewa kuwa changamoto kwani kwao ni baridi na huku Ni joto Sana.

"Tumejiandaa vizuri, tunaifahamu vizuri Sana Yanga kwani nimeiona hata kwenye fainali ya kombe la shirikisho, tumekuja kupambana dakika 90 zitazungumza".

Aidha kupitia kwa kepteni wa ASAS Ntirwaza Sudi amesema wanaijua Yanga licha ya kuwa tofauti na msimu uliopita.

"Tunajua Yanga vizuri, uimara wao ni sehemu ya ulinzi na viungo, msimu huu nafasi ya ushambiliaji hawako vizuri kama msimu uliopita, licha ya kuwa kwenye timu yetu kuna mashabiki wa Yanga na Simba pia ila tutaweka maslahi mbele".

Yanga itacheza mchezo wake wa raundi ya kwanza ligi ya Mabingwa Agosti 20 mwaka huu uwanja wa Azam Complex wakiwa ugenini dhidi ya ASAS ya Djibouti.