Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaweka wazi dili la Fei Toto Azam

Muktasari:

  • Yanga ilimuuza Feitoto kwa Azam FC kwa dau lililofichwa kwa pande hizo mbili, lakini waliwekeana vipengele ambavyo timu hizo zitaendelea kunufaishana kwa mchezaji huyo.

KLABU ya Yanga imetangazo mapata ya mauzo ya wachezaji waliyowapata msimu uliyopita huku mchezaji aliyeuzwa ni kiungo Feisal Salum

Yanga ilimuuza Feitoto kwa Azam FC kwa dau lililofichwa kwa pande hizo mbili, lakini waliwekeana vipengele ambavyo timu hizo zitaendelea kunufaishana kwa mchezaji huyo.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa klabu hiyo Mkurugenzi wa Fedha, Sabri Sadick amesema bajeti ya mapato na matumizi iliyotumika msimu uliopita huku akitaja mapato waliyoyapata kwa upande wa mauzo ya wachezaji ni Sh200 milioni kwa mchezaji Feisal Salum 'Fei Toto' kwenda Azam ambapo awali dili lake halikuwekwa wazi.

"Mauzo ya wachezaji ni Sh200 milioni kama mnavyojua tumeweza kumuuza Feisal Salum 'feitoto" amesema Sabri

Feisal amesaini mkataba wa miaka mitatu, ambao utamfanya akae kwenye timu hiyo ya Chamazi hadi 2026.