Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haji Mnoga kuanza na Carabao Cup

MNOGA Pict

Muktasari:

  • Ratiba inaonyesha Salford, ambayo inaanza kwenye raundi ya kwanza ya mashindano hayo makubwa England, itakipiga na Rotherham United Agosti 12.

NYOTA wa Kitanzania, Haji Mnoga na klabu yake ya Salford City wataanza msimu wa 2025/26 kwa kushiriki mashindano ya Carabao Cup yanayotarajiwa kuanza Agosti mwaka huu.

Ratiba inaonyesha Salford, ambayo inaanza kwenye raundi ya kwanza ya mashindano hayo makubwa England, itakipiga na Rotherham United Agosti 12.

Endapo watafuzu hadi raundi ya pili, huenda wakakutana na timu kutoka Ligi Kuu au Championship.

Kama Salford itatinga hatua inayofuata na kukutana na mojawapo ya timu za Ligi Kuu, basi itakuwa mara ya pili kwa Mnoga kucheza dhidi ya timu ya EPL.

Mara ya kwanza ilikuwa Januari mwaka huu ambapo Salford ilicheza na Manchester City kwenye Uwanja wa Etihad katika mchezo wa raundi ya tatu ya Kombe la FA. Mnoga alicheza kwa dakika 58, ingawa timu yake ilifungwa mabao 8-0.

Ligi ya England imetamatika na Salford, inayomilikiwa na nyota wa zamani wa Manchester United, David Beckham na Garry Neville, ilimaliza katika nafasi ya nane. Kwenye mechi 46, ilishinda 18, sare 15 na kupoteza 13, ikikusanya pointi 69.

Huu utakuwa msimu wa pili kwa Mtanzania huyo kuichezea Salford ya England, akitokea Aldershot aliyoiwakilisha kwa misimu miwili.

Mnoga alicheza mechi 39 kati ya 46 zilizochezwa na timu hiyo, kwa jumla ya dakika 3,306, akiwa ni mhimili mkubwa wa kikosi hicho.

Tangu aliposajiliwa, amekuwa beki wa pembeni tegemeo na kuwaweka benchini nyota mbalimbali kwenye nafasi hiyo. Alifunga bao moja na kutoa asisti nne za mabao.