Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yawaonyesha Waghana

Wachezaji wa Yanga.

Muktasari:

Sasa sikia. Kumbe jamaa licha ya kwamba wana udhamini wa Kampuni ya Madini kumbe hamna kitu bwana, Yanga wamewaonyesha advataizi moja ya hatari nje ya uwanja kuwadhihirishia kwamba lazima Jumamosi wapigwe Taifa na kwamba wao ndio wawakilishi wa Tanzania inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli na hapa ni kazi tu.

MEDEAMA wanacheza na Yanga kesho Jumamosi saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa. Hakuna ubishi mchezo huo utaonyeshwa na Azam Tv. Fungu la kwanza la Waghana hao lilitua Dar es Salaam jana na jingine litakuja leo Ijumaa.

Sasa sikia. Kumbe jamaa licha ya kwamba wana udhamini wa Kampuni ya Madini kumbe hamna kitu bwana, Yanga wamewaonyesha advataizi moja ya hatari nje ya uwanja kuwadhihirishia kwamba lazima Jumamosi wapigwe Taifa na kwamba wao ndio wawakilishi wa Tanzania inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli na hapa ni kazi tu.

Nyota wa Yanga, Donald Ngoma analipwa Dola 4,000 (Sh 8.4 milioni) kwa mwezi na kuwa miongoni mwa nyota wanaolipwa fedha nyingi klabuni hapo, lakini imebainika mkwanja huo ni mishahara ya wachezaji 11 wa Medeama ambayo itacheza na Yanga kesho Jumamosi.

Taarifa zilizopatikana Ghana ni kwamba mchezaji ghali zaidi katika ligi ya nchi hiyo analipwa Dola 600 (Sh 1.2 milioni) na hata hivyo hayupo Medeama, bali Heart of Ouk iliyowahi kunolewa na kocha wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic.

Kwa upande wa Medeama nyota wanaolipwa mkwanja mnene ni nahodha wao na kipa Muntari Tagoe na kiungo, Maliki Akowuah wanaolipwa Cedis 1500 za Ghana ambazo ni sawa na Dola 385 (Sh 810,000).Nyota wengine klabuni hapo wanalipwa kati ya Dola 150 (Sh 320,000) hadi 350 (Sh 715,000) fedha ambazo kwa Yanga zinaonekana kuwa za chai tu kwa wachezaji tena kwa siku moja wakienda kufanya mazoezi pale Boko. Kwa hesabu hiyo ni kwamba mshahara wa Ngoma unaweza kuwalipa nyota 11 wa Medeama na mwingine mmoja wa benchi.

Rais wa Heart of Ouk, Odotei Sowah aliiambia Radio Nhyira FM ya nchini humo kuwa, klabu yake ndiyo inayofanya malipo makubwa zaidi Ghana na kuwapiku hadi wapinzani wao wakubwa Asante Kotoko.

“Kwa upande wa mishahara Hearts inalipa zaidi kuliko timu nyingine, tunalipa vizuri zaidi ya hata wapinzani wetu Asante Kotoko, mfano kwetu wapo tunaowalipa hadi Dola 600 (Sh 1.3 milioni), hakuna klabu nyingine inayoweza kulipa hivyo,” alisema Sawah.

Mwandishi wa habari za michezo nchini Ghana, Evans Antwi aliliambia Mwanaspoti kuwa hali ya wachezaji Ghana ni ngumu na ndio maana Medeama inasuasua na kutaka kujitoa Kombe la Shirikisho.