Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yatesa tuzo za ligi Kuu Bara

Muktasari:

Straika Ibrahim Ajib wa Simba aliibuka kidedea katika tuzo ya bao bora akimbwaga, Amisi Tambwe wa Yanga. Mabao yaliyompa ulaji Ajib ni lile la pili dhidi ya Azam katika matokeo ya 2-2 na jingine ni dhidi ya Mgambo alipofunga kwa kuwachambua mabeki. Ajib pia amelamba Sh 3 Milioni.


 WAKATI kocha Hans Pluijm wa Yanga akiibuka kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) Bara msimu wa 2015/16, beki wa timu hiyo, Juma Abdul ametwaa tuzo ya mchezaji bora.

Tuzo hizo zilitolewa jana Jumapili jijini Dar es Salaam ambako Pluijm pia amelamba Sh 8 Milioni na kukabidhiwa tuzo na Mwenyekiti wa Chama cha Makocha (Tafca), Dan Koroso. 

Kocha huyo Mholanzi alikuwa akiwania tuzo hiyo na Mecky Maxime wa Mtibwa Sugar ambaye sasa amehamia Kagera Sugar na Salum Mayanga wa Prisons.  

Kwa upande wa mchezaji bora, Juma Abdul aliwabwaga Shiza Kichuya wa Mtibwa ambaye ametua Simba na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ wa Simba. Abdul alikabidhiwa tuzo hiyo na mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, tuzo ambayo inaambatana na Sh Milioni 9.2 Milioni. 

Straika Ibrahim Ajib wa Simba aliibuka kidedea katika tuzo ya bao bora akimbwaga, Amisi Tambwe wa Yanga. Mabao yaliyompa ulaji Ajib ni lile la pili dhidi ya Azam katika matokeo ya 2-2 na jingine ni dhidi ya Mgambo alipofunga kwa kuwachambua mabeki. Ajib pia amelamba Sh 3 Milioni.

Aishi Manula wa Azam aliwabwaga Deogratius Munishi ‘Dida’ wa Yanga na Ben Kakolanya wa Prisons ambaye amehamia Yanga pamoja na Vincent Angban wa Simba na kutwaa tuzo ya kipa bora. Manula alikabidhiwa tuzo hiyo na kipa wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Mohammed Mwameja, tuzo ambayo inaambatana na Sh 5.7 Milioni.

Katika kipengele cha mchezaji bora wa kigeni, Thaban Kamusoko wa Yanga aliwabwaga Angban wa Simba na Donald Ngoma wa Yanga. Kamusoko pia amelamba Sh 5.7 Milioni.

Straika Mrundi wa Yanga, Amisi Tambwe ametwaa tuzo ya mfungaji bora kwa mabao yake 21, tuzo hiyo alikabidhiwa na straika wa zamani wa Yanga, Simba na Taifa Stars, Mohammed Hussein ambaye rekodi yake ya mabao 26 ya ligi kuu haijavunjwa hadi sasa. Tambwe pia amelamba Sh 5.7 Milioni.

Katika kinyang’anyiro cha timu yenye nidhamu JKT Ruvu, Mgambo Shooting na Mtibwa Sugar zilichuana ambako Mtibwa iliibeba tuzo hiyo na kupokewa na Maxime. Tuzo hiyo inaambatana na Sh 17.2 Milioni.

Mbio za tuzo ya mwamuzi bora, mchuano ulikuwa kati ya Anthony Kayombo, Ngole Mwangole na Rajab Mrope. Mwangole aliibuka kinara ambaye pia amelamba Sh 5.7 Milioni. 

Tshabalala wa Simba alitwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi akiwabwaga Farid Mussa wa Azam na Shiza Kichuya wa Mtibwa ambaye kwa sasa amehamia Simba. Tshabalala pia alilamba Sh 4 Milioni.

Kabla ya utoaji wa tuzo  hizo, vinara wa ligi, Yanga, Azam walioshika nafasi ya pili, Simba ya tatu na Prisons ya nne wote walipewa tuzo zao. Yanga walilamba Sh 81 Milioni, Azam Sh 40.6 Milioni, Simba Sh 29 Milioni na Prisons Sh 23.2 Milioni.