Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bodi ya Ligi: Kariakoo Dabi ipo palepale

DABI IPO Pict

Muktasari:

  • Akitangaza hayo mchana huu Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi Almas Kasongo amesema bodi yao imeyapokea na kwenda kuyafanyia kazi huku akisisitiza kwamba mchezo huo wa Juni 15, 2025 upo palepale.

BODI ya Ligi Tanzania TPLB imesema katika mkutano wao na Yanga, klabu hiyo imekuja na mambo manne ambayo inataka yafanyiwe kazi kabla ya mchezo dhidi ya Simba.

Akitangaza hayo mchana huu Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi Almas Kasongo amesema bodi yao imeyapokea na kwenda kuyafanyia kazi huku akisisitiza kwamba mchezo huo wa Juni 15, 2025 upo palepale.

Kwenye hoja hizo Kasongo amezitaja kwamba Yanga imetaka Kamati ya usimamizi wa Ligi ivunjwe sambamba na kujiuzulu kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo.

Amesema pia Yanga imetaka Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF Wilfred Kidao naye ajizulu huku mwisho ikitaka Bodi ya Ligi iwe chombo huru.

"Tumekutana na Yanga kilikuwa ni kikao kizuri chenye kujenga, kama mnavyofahamu TPLB ni chombo cha klabu na tunapokutana ni jambo lenye afya,"alisema Kasongo

"Tumeyapokea mambo manne ambayo wameyaleta na sisi kama TPLB hatua ya kwanza tumeyapokea na baada ya kuyapokea tutakwenda kuyachakata.

"Kwenye haya mambo manne ni jambo moja ambalo lipo kwenye mamlaka ya Mwenyekiti wa Bodi ambalo ni muundo wa Kamati ya usimamizi wa Ligi lakini haya mengine yanahitaji muda na kuamuliwa kwenye vyombo vingine tofauti.

"Haya yanahitaji muda kuweza kupata muafaka wake hayawezi kufanyika kwa haraka hata kama ukitaka kuyafanyia kazi kwa hiyo kwa mamlaka yangu au wa nafasi yangu naweza kusema ratiba inabaki vilevile kama ambavyo ilipangwa mpaka hapo itakapoamuliwa vingine."