Yanga yatafuta pointi sita kwa Azam FC, Ruvu Shooting

Muktasari:
- Bao la Yanga lilifungwa na Thaban Kamusoko katika kipindi cha kwanza dakika ya 26 na kukifanya kikosi hicho kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza.
Dar es Salaam. Timu ya Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Bao la Yanga lilifungwa na Thaban Kamusoko katika kipindi cha kwanza dakika ya 26 na kukifanya kikosi hicho kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza.
Yanga imevunja mwiko wa kupoteza mechi zake tisa mfululizo baada ya mchezo wake uliopita pia kutandikwa bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC mkoani Shinyanga.
Ushindi huo wa Yanga unawafanya kufikisha pointi 51 wakiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Kamusoko alisema malengo ya timu hiyo ni kuibuka na ushindi kwa mechi zote zilizosalia huku wakiwa na kibarua kwa Azam FC pia Ruvu Shooting.