Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

QPR ya England yamalizana na beki Mbongo

QPR Pict

Muktasari:

  • QPR imemsajili beki huyo wa kulia raia wa Australia kutoka Macarthur FC ya Sydney kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika Juni 30 mwaka huu.

HATIMAYE, baada ya tetesi za muda mrefu kuwa QPR ya England inahitaji huduma ya beki Adamson Kealey, imemsajili rasmi nyota huyo mwenye asili ya Tanzania.

QPR imemsajili beki huyo wa kulia raia wa Australia kutoka Macarthur FC ya Sydney kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika Juni 30 mwaka huu.

Adamson, mwenye umri wa miaka 22, amecheza mechi 38 kwenye Ligi Kuu ya Australia (A-League) akiwa na Macarthur, na kufunga mabao mawili.

Akizungumza na tovuti ya klabu ya QPR, Adamson alisema:

“QPR ni klabu kubwa sana na ya muda mrefu yenye historia kubwa. Hata tukiwa Australia, naamini kila mtu anajua kuhusu QPR. Ni klabu ya kuvutia sana, inaungwa mkono vizuri na orodha ya sifa zake ni ndefu. Mimi niko tayari kuanza kazi mara moja.”

QPR, ambayo kirefu chake ni Queens Park Rangers na pia maarufu kama The Hoops, itaanza msimu wa Ligi ya Championship 2025/26 kwa mchezo wa nyumbani dhidi ya Preston North End, Agosti 9.

Nyota huyo pia ni mshindi mara mbili wa Kombe la Australia (Australia Cup), kwanza akiwa na Sydney FC na baadaye .akiwa na Macarthur.