Yanga yashusha mziki, Simba yapangua wawili

Yanga yashusha mziki, Simba yapangua wawili

Muktasari:

  • Baadhi ya nyota walikuwa wamekosekana kwa sababu mbalimbali wakiwa ni Khalid Aucho, Ducapel Moloko, Saido Ntibazonkiza, Khalid Aucho na Feisal Salum.

Vinara wa Ligi Kuu Bara wameachia kikosi chao kitakachoanza kwenye mechi dhidi ya watani zao Simba kwenye mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Katika mechi kadhaa zilizopita Yanga waliwakosa baadhi ya nyota wao wa kikosi cha kwanza kutokana na sababu mbalimbali ila leo wameshusha fulu mziki.

Baadhi ya nyota walikuwa wamekosekana kwa sababu mbalimbali wakiwa ni Khalid Aucho, Ducapel Moloko, Saido Ntibazonkiza, Khalid Aucho na Feisal Salum.

Katika mechi ya leo itakayoanza muda mfupi kuanzia sasa nyota hao wote waliokosekana katika baadhi ya mechi wameanza katika mchezo huu wa Dabi kubwa Afrika.

Kikosi cha Yanga kimeanza na Djugui Diarra, Djuma Shabani, Kibwana Shomary, Bakari Mwamnyeto na Dickson Job wanaocheza katika nafasi ya ulinzi.

Kwenye eneo la kiungo wapo, wawili Yanick Bangala na Khalid Aucho, ambao watacheza kwenye nafasi ya kiungo wazuiaji.

Kwenye eneo la kiungo cha ushambuliaji wapo, Saido Ntibazonkiza, Feisa Salum na Ducapel Moloko huku mshambuliji atakuwa Fiston Mayele.

Mayele anatazamwa kwenye mechi hii kama mchezaji wa kuchungwa zaidi kwani ndio kinara wa ufungaji katika Ligi Kuu Bara hadi sasa akiwa na mabao 12.

Kwenye benchi la akiba wapo, Aboutwalib Mshery, Yassin Mustapha, Ibrahim Abdallah, Zawadi Mauya, Salum Abubakar, Crispin Ngushi, Heritier Makambo, Denis Nkane na Farid Mussa.


SIMBA YAPANGUA WAWILI
Kwenye kikosi cha Simba kinamabadiliko ya wachezaji wawili walioanza katika mchezo wa mwisho wa kimashindano waliocheza dhidi ya Orlando Pirates ugenini.

Kwenye kikosi cha Simba kilichoanza katika mchezo wa Orlando robo fainali kombe la Shirikisho Afrika, waliotolewa ni Pascal Wawa na Israel Mwenda.

Katika kikosi cha leo kilichoanza dhidi ya Yanga, Wawa hayupo hata kwa wachezaji waliokuwa benchi wakati Mwenda ni miongoni mwa wachezaji tisa wakiokuwa kwenye benchi la akiba.

Kukosekana kwa wachezaji hao wawili kwenye kikosi cha kwanza nafasi zao wamechukua Benard Morrison asiyekwenda Afrika Kusini na Clatous Chama aliyebanwa na sheria kucheza machindano hayo.

Kikosi cha Simba kimeanza na Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein, Inonga Baka waliokuwa kwenye nafasi ya ulinzi.

Kwenye nafasi ya kiungo wapo watatu Jonas Mkude, Sadio Kanoute watakaocheza kwenye eneo la kukaba zaidi na Chama atakuwa juu yao kama kiungo wa kuanzisha mashambulizi.

Washambuliaji watakuwa watatu, Chris Mugalu, Pape Sakho na Morrison anayecheza dhidi ya waajiri wake wa zamani.

Kwenye benchi la akiba wapo, Benno Kakolanya, Mwenda, Rally Bwalya, Erasto Nyoni, Mzamiru Yassin, John Bocco, Kennedy Juma, Yusuph Mhilu na Kibu Denis.