Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yashusha beki usiku mnene, Wakongo waleta kauzibe

Muktasari:

  • Beki huyo aliyetua sambamba na meneja wake akiyokea jiji la Kinshasa, DR Congo amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili ni kati ya nyota wapya walioanza kutua nchini kujiandaa na kambi ya maandalizi ya msimu mpya itakayoanza kesho Jumatatu.

SAA chache kabla ya kambi mpya ya Yanga kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano kuanza kesho Jumatatu, mabosi wa klabu hiyo wakimpokea beki wa kushoto mpya, Chadrack Boka usiku mnene wa juzi, huku ikikwepa kiunzi kilichowekwa na FC Lupopo aliyokuwa akiichezea msimu uliomalizika hivi karibuni.

Beki huyo aliyetua sambamba na meneja wake akiyokea jiji la Kinshasa, DR Congo amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili ni kati ya nyota wapya walioanza kutua nchini kujiandaa na kambi ya maandalizi ya msimu mpya itakayoanza kesho Jumatatu.

Boka anayemudu pia kucheza kama winga, alikuwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na FC Lupopo, lakini Yanga iliamua kufanya makubaliano ya kumnunua ili aje kuziba nafasi ya Mkongomani mwenzie Joyce Lomalisa ambaye inaelezwa ameshapewa ‘thank you’.

Taarifa za ndani zinasema, beki huyo ameshawasili tayari nchini tangu usiku wa juzi na sasa kiachosubiriwa ni kutangazwa tu kama ilivyo kwa Prince Dube aliyetokea Azam FC na Jean Baleke aliyewahi kuichezea Simba kabla ya kwenda Libya akiitumikia klabu ya Al Ittihad ya Libya kwa mkopoa akiyokea TP Mazembe.

“Aliingia mjini usiku na kupokelewa na moja kati ya viongozi wa klabu yake hiyo mpya na wakati wowote atajiunga na timu kambini hata kabla ya kutangazwa kwani kila kitu kimeshakamilia juu yake,”€kilisema chanzo hicho kutoka Yanga na kuongeza:

“Kilichobaki kwa beki huyo wa kushoto ni kumtangaza tu, na Yanga itafanya hivyo mapema ili aweze kujiunga na wachezaji wenzake haraka kwa ajili ya maandalizi ya pre season.”€

Beki huyo ametua Yanga kwenda kucheza kushindana na Nickson Kibabage, mzawa aliyeongezewa mkataba hivi keribuni kuendelea kuitumikia timu hiyo aliyokuwa nayo tangu msimu uliopita akiitumikia kwa mkopo akitokea Singida Fountain Gate.


KIUNZI CHA WAKONGO

Awali kulikuwa na taarifa kwamba beki huyo huenda angechelewa kuungana na timu hiyo kutokana na klabu ya FC Lupopo kukimbimbilia Shirikisho la Soka la DR Congo (Fecofa) ili kuzuia kutolewa kwa Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC).

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga kililiambia Mwanaspoti mapema kuwa, mabosi walifanya makubaliano na beki huyo ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili, lakini mambo yamekuwa magumu kutokana na FC Lupopo kuchelewesha kumuachia wakidai sehemu ya malipo.

“FC Lupopo haijataka aondoke kikosini kwao wakidai bado ni mchezaji wao na kukimbilia Shirikisho la Soka la DRC (Fecofa) ikilitaka lisitoe (ITC) kwenda Yanga kwa ajili ya kukamilisha usajili huo,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Mchezaji na wasimamizi (wake) walikuwa wakipambana kutafuta ITC wakati Boka akiwa tayari njiani kuwahi kambi ya Yanga inayoanza Julai 8 (kesho Jumatatu).”

Mchezaji huyo ambaye alifanya vizuri katika Ligi Kuu DR Congo inaelezwa kuwa sio wa FC Lupopo, bali ni wa klabu ya Real of Kinshasa, lakini alijiunga na FC Lupopo kwa mkopo na inaelezwa Yanga wamemalizana na Real of Kinshansa, ila timu aliyocheza msimu ulioisha (Lupopo) inachelewesha ITC.

“Kuna mambo ambayo Lupopo inataka ifanyiwe na Yanga, ilihali tangu mapema tulijulishwa kwamba alikuwa katika klabu hiyo kwa mkopo na tulimalizana na klabu ya Real na menejimenti yake inapambana kuona hiyo kitu inaisha na ITC inatumwa ili Boka aitumikie Yanga kama walivyokubaliana, kwani imemsajili kihalali,” kilisema chanzo hicho kilichosisitiza kutotaka kutajwa jina gazetini.

Hadi sasa Yanga imemtambulisha mchezaji mmoja tu ambaye ni Chama, huku Bakele, Dube na Boka ambao ni kati ya nyota wapya waliosaini Jangwani walikuwa wanasubiri kuachiwa hadharani kuanzia sasa wakati timu ikiingia kambini kesho.

Chama na Baleke inadaiwa wamepewa mkataba wa mwaka mmoja kila mmoja wenye kipengele cha kuongezewa mwingine mambo yakiwa mazuri uwanjani, huku Dube inaelezwa amepewa miwili kama ilivyo kwa Boka na nyota waliosalia kikosini wameongezewa ili waendelee kuitumikia timu hiyo.

Walioongezewa mikataba ni makipa Djigui Diarra na Abuutwalib Mshery; mabeki Nickson Kibabage na Bakar Mwamnyeto; viungo Farid Mussa, Jonas Mkude, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, huku Zawadi Mauya, Metacha Mnata, Joyce Lomalisa, Skudu Makudubela wakipewa ‘thank you’, ilihali Gift Fred, Joseph Guede na Kennedy Musonda wakiwa mbioni nao kupewa mkono wa kwaheri, wakati Denis Mkane inadaiwa huenda akatolewa kwa mkopo.