Yanga yamtaka Rasta wa Simba

Muktasari:
Kiungo Awesu 'Rasta' alivutia Simba wakati wa mchezo robo fainali ya Kombe la Shirikisho Azam uliofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Yanga yamtaka Rasta wa Simba
Bertha Ismail, Mwananchi
Arusha. Yanga imejitosa kuisaka saini ya kiungo wa Madini, Awesu Awesu 'Rasta' anayewani na Simba pia.
Kiungo Awesu 'Rasta' alivutia Simba wakati wa mchezo robo fainali ya Kombe la Shirikisho Azam uliofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Haspope baada ya mechi hiyo alichukua mawasiliano ya kiungo huyo na kuhaidi kufanya mazungumzo wakati wa usajili ukifika.
Akizungumza suala hilo kiungo Awesu 'Rasta' amesema baada ya Simba kumtaka hivi karibuni Yanga wao wamemfuata
"Kuna klabu vingi vinataka kunisajili nyingine za ligi daraja la kwanza na zingine za Ligi Kuu ikiwemo Singida United, Simba na Yanga."
"Niseme wazi sina mpango wa kuchezea ligi daraja la kwanza wala la pili kwa hiyo wasijisumbue bali macho yangu kwa sasa nimelekeleza kwa timu za Ligi Kuu."
"Kwa sasa nina mazungumzo ya mara kwa mara na viongozi wa klabu mbili kubwa nchini wanapishana kila mara kunipigia simu na kuniita tukazungumze."
"Nimetoa nafasi zaidi kwa Simba au Yanga atakayeweka dau zuri pamoja na kuhakikishiwa nafasi ya kucheza nami naahidi sitawaangusha mashabiki wangu na mabosi wangu popote ntakaposajiliwa."