Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yamkosa Mosimane

Kocha Pitso Mosimane raia wa Afrika Kusini ikiwa imepita siku mbili baada ya kuachia barua ya kuthibitisha kuondoka klabu ya Al Ahli ya Saudi tayari amepata timu mpya.

Mosimane ambaye aliipandisha Ahli kucheza Ligi Kuu ikiwa bingwa alivunja mkataba na timu hiyo baada ya kutolipwa mshahara tangu Februari.

Kocha huyo wa zamani wa Mamelodi na Al Ahly tayari amesaini mkataba wa kuinoa Al Wahda ya Falme za Kiarabu (UAE).

"Al Wahda FC imeingia mkataba na kocha Pitso Mosimane kuwa kocha mkuu, bodi ya wakurugenzi inamkaribisha nyumba ya mabingwa," ilieleza taarifa yao

Al Wahda ambao ni mabingwa mara nne wa Ligi Kuu UAE imemaliza nafasi ya tatu msimu ulioisha na haijashida ubingwa tangu 2009/10.

Mosimane alitajwa miongoni mwa makocha ambao majina yao yalikuwa mezani Yanga akiwemo na Florent Ibenge (61), Juan Carlos Garrido (54), Faouzi Benzarti (73), Nabil Maaloul (60) na Omar Najhi kuziba nafasi ya kocha Nasreddine Nabi ambaye hakuongeza mkataba kuinoa Yanga.