Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yalaani vitendo viovu walivyofanyiwa mashabiki wao fainali CAFCC

Muktasari:

  • Klabu hiyo imetoa taarifa yake kulaani vitendo hivyo badaa ya kusambaa kwa picha mjongeo zikionyesha mashabiki hao kufukuzwa uwanjani kushuhudia fainali hiyo ambayo iliisha kwa sare ya bao 1-1, huku RS Berkane ikibeba kombe kwa kuwa na jumla ya mabao 3-1.

Klabu ya Yanga imesikitishwa na kulaani vikali vitendo vya kupigwa, kuchaniwa jezi na kufukuzwa uwanjani kwa mashabiki wao katika mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa kwenye uwanja wa Amaan Complex ukizihusisha klabu za Simba ya Tanznia na RS Berkane ya Morocco.

Klabu hiyo imetoa taarifa yake kulaani vitendo hivyo badaa ya kusambaa kwa picha mjongeo zikionyesha mashabiki hao kufukuzwa uwanjani kushuhudia fainali hiyo ambayo iliisha kwa sare ya bao 1-1, huku RS Berkane ikibeba kombe kwa kuwa na jumla ya mabao 3-1.

Klabu hiyo iemeeleza kuwa inaamini katika uungwana kwenye michezo huku ikiziziomba mamlaka husika kuchukua hatua kali kwa waliohusika kufanya vitendo hivyo viovu.

Aidha klabu hiyo imetoa pole kwa mshabiki walikumbana na kadhia hiyo na kuwataka mashabiki kuendeleza uungwana na kupinga chuku, uhasama baina ya machabiki hapa nchini

“Uongozi wa Young Africans Sports Club umesikitishwa na unalaani vikali vitendo vya kupigwa, kuchaniwa jezi na kufukuzwa uwanjani kwa mashabiki wake katika mchezo wa Fainali wa Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa Tarehe 25/5/2025 katika uwanja wa Amaan, Zanzibar”.

“Young Africans Sports Club tunaamini kwenye uungwana katika mchezo wa soka, hivyo vitendo walivyofanyiwa mashabiki wetu vinapaswa kulaaniwa na Wadau wote wa soka nchini huku tukiziomba Mamlaka husika kuchukua hatua kali kwa wote waliohusika kufanya uhuni huo”.

“Vile vile, Uongozi wa Young Africans Sports Club unatoa pole kwa mashabiki wote waliokumbwa na kadhia hiyo na unawataka mashabiki wote wa Klabu hii, kuendeleza uungwana na kupinga chuki na uhasama unaotaka kujengwa na makusudi baina ya mashabiki hapa nchini”.

“Mwisho, Uongozi unawaomba mashabiki wote wa Yanga kutolipiza kisasi kwa namna yoyote ile na badala yake waendelee kuwakaribisha mashabiki wa timu nyingine kwenye mechi zetu ili tuendelee kufurahia mchezo wa soka huku tukidumisha ustaarabu wetu wa kulinda amani na usalama wa watu wote wanapokuwa uwanjani”.