Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ZFF kujifunza kupitia AFCON 2027

ZFF Pict

Muktasari:

  • Fainali hizo zilizopangwa kufanyika kuanzia Junia 19, 2027 hadi Julai 17, 2027, kwa Tanzania, vitatumika viwanja vya Dar es Salaam, Arusha na Zanzibar.

MWENYEKITI wa Kamati ya Fedha na Mipango wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), Awadh Maulid Mwita, amesema kupitia Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2027, wanaamini watapata fursa ya kujifunza kimichezo na uandaaji wa michuano mikubwa ya aina hiyo.

Kiongozi huyo ameyasema hayo ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji wa AFCON 2027 kwa kushirikiana na Kenya na Uganda.

Fainali hizo zilizopangwa kufanyika kuanzia Junia 19, 2027 hadi Julai 17, 2027, kwa Tanzania, vitatumika viwanja vya Dar es Salaam, Arusha na Zanzibar.

Mbali na hilo la kujifunza, Mwita amesema kutokana na kwamba Zanzibar ni kisiwa cha utalii, kupitia mashindano hayo wanahitaji kujitangaza kimataifa.

Amesema, watakapokuja wachezaji wenye majina makubwa katika mashindano hayo, Zanzibar itazidi kujitangaza zaidi kwani kwa kawaida wachezaji hao wanakuwa na wafuasi wengi kwenye mitandao yao ya kijamii kwa maana hiyo huo utakuwa wakati mzuri kwao.

“Wanapokuja wachezaji wenye majina makubwa AFCON, jicho lote dunia nzima litakuwa lipo Zanzibar, wakati wakiwafuatilia wachezaji hao watapata nafasi ya kuijua zaidi,” amesema.

Vilevile, amesema wachezaji hao wataonesha vitu vyote ambavyo vipo kisiwani hapa na wengine watavutiwa kufika kushuhudia.

Mbali na hilo, amesema uchumi wa nchi utaongezeka kwa sababu timu kubwa zinapokuja zinafanya matumizi mengi kutoka kwa wachezaji na viongozi wao.

Amesema, wanapoizungumzia AFCON kwasasa wanajadili utanuzi wa utalii, ajira na mafunzo mbalimbali kwa kubadilishana utamaduni kutoka kwa watu tofauti.