Yanga wao ni waamuzi tu dhidi ya JKT

Muktasari:
Kabla ya kuja Dodoma, Yanga imetokea kucheza mchezo dhidi ya Namungo wakitoka suluhu uwanja wa Majaliwa Ruangwa.
WAKATI Yanga ikiwa kwenye maandalizi ya mwisho kabla ya kuikabili JKT Tanzania, bado wanalia na maamuzi ya marefa.
Razak Siwa, Kocha wa makipa wa Yanga, amesema kuelekea mchezo huo wa kesho, waamuzi hawatakiwi kurudia makosa kama walivyofanya mchezo dhidi ya Namungo ambao wanaamini walikataliwa bao lao halali.
Siwa ambaye aliongozana na kipa Ramadhani Kabwili kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika uwanja wa Jamhuri leo Jumanne, amesema wao wamejipanga kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.
"Tumejipanga kuibuka na ushindi dhidi ya wapinzani wetu, kutokana na morali waliyonayo lakini isiwe kama mchezo wa Namungo tulipata bao likakataliwa" amesema Siwa.
Kocha huyu Mkenya aliongeza kuwa, hawaangalii mchezaji gani atacheza ama vinginevyo bali wanachojali ni timu ipate ushindi tu mchezo wa kesho.
Imeandikwa na Matereka Jalilu