Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga wameamua, Maximo hataki kubahatisha

Wachezaji wa timu ya Yanga wakiwa mazoezini. Picha na Michael Matemanga

Muktasari:

Katika makabrasha ya Mbrazili huyo kila siku anaingiza jina au kulifuta jingine katika nafasi za uwanjani na anafanya hivyo kutokana na viwango vya

YANGA kweli wameamua. Kocha Marcio Maximo ‘The Chosen One’ hataki kubahatisha na kuanzia sasa kila nafasi katika kikosi chake itakuwa ina watu wa uhakika wasiopungua watatu.

Katika makabrasha ya Mbrazili huyo kila siku anaingiza jina au kulifuta jingine katika nafasi za uwanjani na anafanya hivyo kutokana na viwango vya

wachezaji wake mazoezini. Anayepungua anafutwa katika orodha na ambaye kiwango kinapanda anaingizwa jina. Kocha huyo anayafanya hayo kuhakikisha anakuwa na kikosi imara chenye ushindani uwanjani.

Mwanaspoti lina uhakika na mpango huo wa Maximo ambao utamwezesha kuwa na kikosi imara cha ushindani ambacho kitaweza kupigania pointi tatu katika kila mechi watakayocheza pale pazia la Ligi Kuu Bara litakapofunguliwa.

Tangu alipoanza kuifundisha Yanga Julai Mosi, kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa, Taifa Stars, amekuwa akiwatazama kwa makini wachezaji wote na kuandika majina yao kitabuni pia akifuatilia taarifa za wachezaji wake walio katika timu za taifa; Taifa Stars, Rwanda na Uganda.

Akianzia golini, Maximo katika kabrasha lake amepanga namba moja ni Deo

Munishi ‘Dida’, anafuata Juma Kaseja halafu Ally Mustapha ‘Barthez’ na kinda Said Ally wa kikosi B amewekwa namba nne.

Nafasi nyingine yenye idadi ya wachezaji wanne huku anayetakiwa kucheza akiwa mmoja ni ile ya ushambuliaji ambayo wapo Genilson Santana ‘Jaja’,

Jerry Tegete, Said Bahanuzi na Hussein Javu. Jaja ndiye wa kwanza hapo.

Katika beki ya kulia, Maximo anao Juma Abdul na Salum Telela huku anayeanza akiwa Abdul. Katikati wapo Kelvin Yondani, Pato Ngonyani na Issa

Ngao kutoka Yanga B kama mabeki wa mwisho huku Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Rajab Zahir wakiwa mabeki wa kati wakabaji. Hapo wanaoanza ni Yondani na Cannavaro.

Beki ya kushoto ndipo kuna dosari kidogo kwani Maximo anaye Oscar Joshua na kinda Amos Abel anayetoka kikosi B.

Nafasi ya kiungo mkabaji, Mbuyu Twite ndiye chaguo la kwanza kwa Maximo akifuatiwa na Omega Seme na kinda Mwinyi Ndimbo kutoka Yanga B wakati namba nane kuna watu watatu ambao ni Haruna Niyonzima, Hassan Dilunga na Hamis Thabit.

Kiungo mshambuliaji namba 10 Maximo anataka kuwatumia wachezaji watatu ambao ni Emmanuel Okwi, Nizar Khalfan na Hamis Juma wa Yanga B huku nafasi ya winga ya kulia kuna watu wawili tu akimtanguliza Mrisho Ngasa na Simon Msuva.

Winga wa kushoto yupo Andrey Coutinho pekee mwenye uhakika wa kucheza eneo hilo huku wengine ni vijana kutoka kikosi B. Pia Maximo anataka kuongezwa kiungo mkabaji anatakayewapa changamoto Twite na Omega.

Kocha huyo ameliambia Mwanaspoti kuwa, ameshaukabidhi uongozi mpango huo wa kusaka wachezaji wapya.

“Nimeshakabidhi kila kitu kwa uongozi katika kuyafanyia kazi hayo yote, nataka kuwa na wigo mpana wa kuchagua wachezaji. Kuna maeneo ni kweli nimeona kuna upungufu nafikiri siyo vyema kuweka wazi sana, lakini ninachoweza kusema nimeshawapa taarifa viongozi,” alisema Maximo.

Yanga yatua Kagame

Uongozi wa Yanga umethibitisha kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika

Mashariki na Kati ‘Kombe la Kagame’ ambapo sasa wanajipanga kujua lini watasafiri kwenda Rwanda.

Katibu Mkuu wa Yanga, Benno Njovu, alisema: “Tunataka kuondoka na wachezaji wetu wote, tatizo linakuja hatutaki kuondoka nusu nusu, tunajipanga kuangalia tunafanyaje hasa ukizingatia kuwa kuna wachezaji wetu wapo katika timu za taifa ambao ni lazima tuondoke nao.”

Michuano hiyo imepangwa kufanyika Rwanda kuanzia Agosti 8.